Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari - 06/03/2020

Uturuki inadai kwamba mhamiaji aliuawa kutokana na vurugu mpakani mwa Ugiriki

Mzozo wa Afghanistan: Amerika Imefanya Shambulizi la Kwanza la Angani dhidi ya Taliban tangu Makubaliano

Kwa Nini Waislamu Wanashambuliwa nchini India

Maelezo:

Uturuki inadai kwamba mhamiaji aliuawa kutokana na vurugu mpakani mwa Ugiriki

Maafisa wa Uturuki walisema kwamba mtu mmoja alijeruhiwa vibaya baada ya vikosi vya usalama vya Ugiriki kutumia silaha za moto kuwapiga wahamiaji waliokua wamekusanyika katika mpaka mnamo Jumatano. Na kwa haraka kabisa Ugirik ilipinga hilo na kudai kwamba haijahusika na tukio lolote la silaha za moto dhidi ya wahamiaji. Maelfu ya watu wameelekea katika mpaka baada ya Uturuki kutangaza kwamba haitawazuia tena wahamiaji wanaohitaji kuvuka mpaka. Pia Ugirirki imekanusha kwamba watu wawili kutoka Syria walijeruhiwa vibaya kwa risasi baada ya kutaka kuvuka mpaka wakati wa usiku. Picha za video zilizopigwa karibu na kaskazini mwa mpaka wa Uturuki na Ugiriki mnamo Jumatano zilionyesha mamia ya wahamiaji wakikimbia mabomu ya gesi. Kundi la watu lilionekana likiwa limembeba mtu katika shuka akiwa amejeruhiwa kichwani, mtu mmoja aliyekuwa akizungumza lugha ya Kifursi alisikika katika video hiyo akisema wanajeshi wa Ugiriki wanawapiga risasi na wahamiaji watano wamejeruhiwa vibaya. Mamlaka ya mji mdogo uliojirani ya Edirne ilichapisha taarifa inayosema mtu mmoja amefariki na wengine watano wamejeruhiwa vibaya. Taarifa hiyo ili walaumu askari wa Ugiriki na vikosi maalumu vya mpakani kwa kuwarushia risasi wahamiaji wakiwa katika eneo salama baina ya lango la mpakani la Ugiriki la Kastanies na lango la Uturuki la Pazakule. Msemaji wa serikali ya Ugirki Stelios Petsas alinukuliwa akisema kwa hasira "hakukuwa na tukio hilo la urushaji wa risasi kutoka kwa mamlaka za Ugiriki" na kuilaumu Uturuki kwa "kutengeneza na kusambaza habari za uongo". Watu watatu kutoka Afghanistan na Senegal walimwambia muandishi wa habari wa BBC Jonah Fisher kuhusu tukio lililotokea mapema siku ya Jumanne usiku kwamba waliwaona Wasyria wawili wamepigwa risasi ma kujeruhiwa vibaya shingoni na kichwani. [Chanzo: BBC News]

Ni aibu kubwa kuona kwamba Erdogan anawatumia wahamiaji Wasyria na Waislamu wengine kama karata dhidi ya EU. Erdogan angeliweza kumaliza janga la wahamiaji kwa kuiteka Syria na kuifanya kuwa ni sehemu ya Uturuki.

Mzozo wa Afghanistan: Amerika Imefanya Shambulizi la Kwanza la Angani dhidi ya Taliban tangu Makubaliano

Jeshi la Amerika limefanya shambulizi la angani dhidi ya wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan, ikiwa ni saa chache tu tangu Rais Donald Trump aliposema kwamba "nimekuwa na mazungumzo mazuri sana" na kiongozi wa Taliban. Amerika iliweka saini kwa makubaliano na Taliban mnamo Jumamosi yaliyolenga kuleta amani nchini Afghanistan baada ya miaka mingi ya vita. Lakini msemaji wa vikosi vya Amerika alisema wamefanya shambulizi la angani mnamo Jumatano ikiwa ni jibu kwa wapiganaji wa Taliban waliokuwa wakipigana na vikosi vya Afghan katika mkoa wa Helmand. Taliban inataka upunguzaji vita. Kupitia Twitter, Suhail Shaheen msemaji wa Taliban alisema, "tunapanga kutekeleza kila nukta tuliyokubaliana ili kuzuia kuzidi kwa mzozo." Na aliongeza kusema, "Na upande wa pili pia uondoshe vikwazo vyote vinavyozuia utekelezaji wa nukta zote za makubaliano ili kutoa mwanya wa amani kamilifu na Waafghan waweze kupata haki zao msingi." Bado haijakuwa wazi kama shambulizi la Jumatano lilisababisha majeruhi. Shambulizi la Jumatano ni la kwanza la Amerika dhidi ya Taliban ndani ya siku 11 tangu kuanza kwa makubaliano ya kupunguza vurugu baina ya pande mbili na kupelekea katika mkataba wa Jumamosi. Kupitia Twitter, Kanali Sonny Leggett, msemaji wa vikosi vya Ameriki nchini Afghanistan alisema. "lilikua ni shambulizi la kujilinda " ili kuzuia shambulizi kwa Vikosi vya Usalama wa Taifa vya Afghan katika kituo cha ukaguzi. Msemaji huyo aliongezea kwamba Amerika bado "inazingatia amani" lakini pamoja na hilo bado tunawajibu wa kuwalinda washirika wetu Waafghan. Alisema Waafghan na Amerika wamejifunga na upande wao katika makubaliano, ilhali Taliban inaonekana kama ambaye inataka “kuharibu” fursa hiyo. [Chanzo: BBC News]

Kwa maraa nyingine tena, Amerika inaonyesha kutoheshimu makubaliano iliyosaini na nchi nyingine. Amerika ilijitoa katika mkataba wa nyuklia na Iran, na ikajitoa katika mkataba wa INF iliyosaini na Urusi na hivi sasa imeshavunja mkataba mchanga iliosaini na Taliban. Ama Taliban, walikuwa katika upande wenye nguvu na wasingelijisalimisha kwa mpango wa Amerika usiokuwa na maana. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ]

“Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mkatakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.” [TMQ: 47:35]

Kwa Nini Waislamu Wanashambuliwa nchini India

Watu 46 hadi wameuawa, na zaidi ya 250 wamejeruhiwa vibaya na misikiti 4 kuchomwa moto katika vurugu za kidini zilizotokea Delhi ambazo zilisadifiana na ziara ya Rais Trump nchini India. Vurugu hizo, zilidumu zaidi ya siku tatu mchana na usiku na la kutoshangaza ziliwalenga zaidi Waislamu wa maeneo ya kaskazini mashariki ya Delhi. Zaidi ya miaka sita, Waziri Mkuu Narendra Modi na wenzake wake ndani ya chama cha Kitaifa cha Kihindu cha Bharatiya Janata, kupitia kwa majeshi yao katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakikuza chuki hizi na kuandaa tuhuma na vurugu dhidi ya Waislamu walio wachache nchini India. Hali hiyo ya kuogofya iliyotokea Delhi ilifuatia baada ya kupitishwa sheria ya ubaguzi ya uraia na serikali ya Modi mnamo Disemba. Wahindi, hususan Waislamu, walikuwa wakiandamana dhidi ya sheria hiyo. Kabla ya mauaji ya Delhi, watu19 waliuawa pindi maandamano yalipoanza katika mji jirani wa Uttar Pradesh, ambao unaongozwa na chama B.J.P. B.J.P. kilishindwa katika uchaguzi uliofanyika Delhi na maandamano yaliendelea. Mnamo Februari 23, Kapil Mishra, kiongozi wa B.J.P aliyachochea magenge kaskazini mwa Delhi kuliondosha kundi la wanawake Waislamu ambao walikuwa wamefunga barabara kwa maandamano dhidi ya sheria ya uraia. Vurugu ikaanzia hapo. Maafisa wa ngazi za juu walidhihirisha wazi uungaji mkono magenge na hofu yao dhidi ya Waislamu. “Jai Shree Ram,” ni wimbo wa kujitolea wa zamani kumsifu Ram, mungu wa Wahindu katika kupigia debe vita miongoni mwa magenge ya Kihindu ya kitaifa ndani ya miongo mitatu iliyopita. Kuna ripoti zinadai kwamba maafisa wa polisi wa Delhi wamekuwa wakiingia katika nyumba za Waislamu huku wakitamka kwa kelele “Jai Shree Ram!”. Tabia hii ya kiubaguzi ya maafisa wa Delhi sio tu suala la polisi bali linadhihirisha migawanyiko iliyomo ndani ya watu ambao wameajiriwa kutokana nao. Ni muendelezo wa kudumu katika tabia hiyo wanayoiamini kuwa itazawadiwa na serikali ya Modi na chama tawala. Maafisa wa polisi waliotekeleza vurugu hawatokabiliwa na hatua za kisheria. Inawezekana hawakutenda kwa mujibu wa Katiba, lakini walisimama na B.J.P. Inatarajiwa kuwa magenge ya Wahindu yatakapo walenga Waislamu katika sehemu yoyote ya nchi inayosimamiwa na chama cha Modi, tunahakika kwamba hakuna polisi ambaye atayapinga. [Chanzo: Gulf News]

Utawala wa Modi unadhibiti kiukamilifu vyombo vya habari vyote na vikosi vya usalama, na hili linafanya kuwa ni wepesi kwa Modi kupitisha mfumo wake wa kiubaguzi ambao daima unawabagua Waislamu. Licha ya mashambulizi haya, watawala kiuwazi wanamkaribisha Modi katika ulimwengu wa Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاء تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءكُم مِّنَ الْحَقِّ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni …” [TMQ: 60:1]

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Machi 2020 09:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu