Jibu la Swali: Mazungumzo ya Usaliti Kati ya Lebanon na Umbile la Kiyahudi
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jijini Washington, mazungumzo yalifanyika kati ya mabalozi wa Lebanon na umbile la Kiyahudi. Hii ilionekana kama mazungumzo ya kiwango cha juu cha amani, pamoja na makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku kumi ambayo baadaye yaliongezwa hadi miezi mitatu mnamo Aprili 24, 2026. Hata hivyo, umbile la Kiyahudi linaendelea kuzidisha uchokozi wake, “jeshi la uvamizi lilitangaza kwamba lilifanya mfululizo wa mashambulizi usiku kucha likilenga zaidi ya maeneo hamsini kusini mwa Lebanon...” (Al-Jumhur, Mei 2, 2026). Je, nia, kama Trump alivyosema, ni amani kupitia nguvu? Basi watawala wa Lebanon wanawezaje kukubali mazungumzo haya ya usaliti ambayo waziwazi, na si kwa siri, yanamaanisha kupanda treni ya uhalalishaji mahusiano?



