Jumatatu, 21 Dhu al-Qi'dah 1446 | 2025/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

India, Pakistan, na Usitishaji Mapigano
(Imetafsiriwa)

Swali:

Trump alitangaza kwa mshangao jana, Jumamosi, katika chapisho kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Kijamii (Truth Social platform), kwamba "Baada ya usiku mrefu wa mazungumzo yaliyopatanishwa na Marekani, ninafurahi kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubali kusitishwa kwa mapigano kamili na mara moja, "na kuzisifu nchi zote mbili kwa kutumia busara na akili kubwa." (Al Jazeera, 11/5/2025) Taharuki ilikuwa imeongezeka kati ya India na Pakistan kufuatia shambulizi la watalii katika Bonde la Baisaran katika eneo la Pahalgam la Jammu na Kashmir linalotawaliwa na India mnamo tarehe 22/4/2025, ambalo liliua Wahindi 25 na Mnepali mmoja. Mnamo 23/4/2025, India ilitangaza kusimamishwa kwa Mkataba wa maji wa Indus 1960  kama sehemu ya msururu wa hatua za adhabu dhidi ya Pakistan. Katika kujibu, Pakistan ilitangaza kusitishwa kwa Makubaliano ya Shimla wa 1972, ambayo yanasimamia mahusiano ya nchi hizo mbili. Mnamo Mei 7, India ilitangaza utekelezaji wa operesheni ya kijeshi inayoitwa "Operesheni Sindhur"... kisha Pakistan ikajibu... na sasa, huku Trump ametangaza kuwa upatanishi wake umefaulu katika kufikia usitishaji mapigano... ni upi ukweli katika uhasama na mzozo huu? Je, Mkataba wa Maji wa Indus ni nini haswa ambao India imeusitisha kwa muda? Je, Marekani inahusika katika kuanzisha shambulizi hilo na pia kulisitisha?

Jibu:

Ili kufafanua jibu la maswali haya, ni muhimu kuhakiki ukweli ufuatao:

1- Chama cha Bharatiya Janata, kilichoingia madarakani nchini India chini ya uongozi wa Atal Bihari Vajpayee kuanzia 1998 hadi 2004, na kisha kurejea madarakani chini ya Narendra Modi mnamo 2014 baada ya miaka 10 ya utawala wa chama kinachounga mkono Uingereza, ni chama kinachounga mkono Amerika kama sehemu ya mkakati wake wa Eurasian kukabiliana na China, yaani, ni wazi kwamba maslahi ya haraka ya Amerika katika Mashariki ya Mbali yalikuwa nyuma ya ushindi wa Mbabe wa Kibaniani Modi mnamo 2014, na inaendelea kumuunga mkono. Narendra Modi amekuwa akitumikia maslahi ya Amerika kila wakati, iwe katika kuunganishwa kwa Kashmir mnamo 2019, au katika mapigano ya mpaka aliyoshiriki na China mnamo 2014, 2017, na 2020, au Afghanistan, au kwa kutofaulu kwa Ukanda wa Uchumi wa China-Pakistan.

2- Baada ya Modi kuingia madarakani nchini India mwaka wa 2014, Marekani ilitumia vyema India kuongeza shinikizo kwa China, kuizunguka, kuizuia kudhibiti maeneo yanayoizunguka, na kuifungia ndani ya eneo lake. Hii ni kweli hasa kwa vile Marekani imetangaza vita vya kiuchumi dhidi ya China, huku Trump akilazimisha ushuru mkubwa kwa bidhaa za China. Kupitia ushuru huu wa ziada, Trump analenga kudhoofisha uchumi wa China. Habari zimeenea kwamba makampuni makubwa ya teknolojia, kama vile iPhone, yananuia kuhamishia viwanda vyao nchini India kutokana na ongezeko kubwa la ushuru. "Apple ilifichua kuwa inapanga kuhamisha uunganishaji wa iPhones zote zinazouzwa nchini Marekani hadi India, kwa mujibu wa Financial Times." (Euro News, 26/4/2025). Kwa hivyo, kama sehemu ya mkakati wake wa kukabiliana na China, Marekani inataka kuimarisha wadhifa wa India kama nguvu ya kiuchumi na kijeshi katika eneo hilo.

3- Hili lilihitaji, kwa upande mmoja, kuunga mkono India kwa njia za kijeshi na kiuchumi, na, kwa upande mwingine, kutatua matatizo ya India na Pakistan, ambapo tawala zote mbili ni tiifu na vibaraka wa Amerika, ili India iweze kushughulika na upande wa China.

Ama kwa upande wa kwanza, Amerika iliunga mkono India na jeshi lake kwa njia zote, kama vile kuhamisha teknolojia ya nyuklia ya Amerika kwenda India. Suala la kukabiliana na China lilijitokeza sana wakati wa mkutano wa Trump na Waziri Mkuu wa India jijini Washington: "Viongozi hao wawili pia walijadili kuimarisha muungano wa usalama wa kundi la Quad katika eneo la Asia-Pasifiki, ambalo pia linajumuisha Japan na Australia. India imepangwa kuwa mwenyeji wa viongozi wa kundi hili baadaye mwaka huu, ambayo inaonekana kama kukabiliana na kuongezeka kwa shughuli za kijeshi za China." (Reuters, 14/2/2025).

Upande wa pili ulikuwa ndio tatizo kuu zaidi kati ya matatizo haya:

a- Vikosi vya Pakistan mpakani vinazuia harakati za vikosi vya India dhidi ya China. Kwa hiyo, Marekani iliisukuma Pakistan kuhamisha majeshi yake kutoka mpaka wa India hadi maeneo ya kikabila ya Waziristan ili kupigana na Taliban wa Pakistan, kwenda Balochistan kupigana na Jeshi la Ukombozi la Balochistan, na mpaka wa Afghanistan. Hii ni kuruhusu India kusonga mbele ikiwa huru dhidi ya China na kuhamisha majeshi yake kwenye mpaka wa China badala ya kupeleka kwenye mpaka wa Pakistan. Kisha Marekani ilianza kuitaka Pakistan kufanya makubaliano na India ili kuwezesha India kujiondoa katika makabiliano na Pakistan na kuiweka katika makabiliano na China. Kwa ajili hiyo, kama tulivyotaja hapo awali, Pakistan ilihamisha vitengo vyake vingi ya kijeshi kutoka kwenye mpaka na India na kuwatumia katika mapigano ya ndani ya Pakistan dhidi ya makundi ya kijihadi... na kuanza kupigana na Taliban nchini Afghanistan.

b- Mzozo juu ya Kashmir, ambayo India iliiunganisha kwake kupitia uamuzi wake mnamo 5/8/2019

Tulisema katika Jibu la Swali, 18/8/2019

(...Muda mfupi baada ya matukio ya Septemba 11, 2001, utawala wa Bush uangazia India. Sehemu kubwa ya hatua za Marekani zilielekezwa katika kuziba pengo la kijeshi kati ya India na China, kwa mujibu wa mipango ya Marekani ... kutokana na hatua hizi ni makubaliano ya nyuklia ya Amerika na India.

Amerika iliona kwamba taharuki juu ya Kashmir kati ya India na Pakistan inaathiri kudhoofisha makabiliano ya Bara ndogo la India dhidi ya China ... Ili kuondokana na taharuki hii, Marekani ilianza mchakato wa kuhalalisha mahusiano kati ya India na Pakistan, na lengo la kuhalalisha mahusiano hayo lilikuwa ni kuondosha majeshi ya India na Pakistan dhidi ya kupigana kwa sababu ya Kashmir, na kuelekeza juhudi kuelekea ushirikiano na Marekani hatimaye kuzuia kuinuka kwa China. Marekani iliamini kwamba kuunganishwa kwa Kashmir kwa India na shinikizo la Amerika kwa utawala wa Pakistan kuuzuia kuchukua hatua za kijeshi na kuigeuza mada hii kwenye mazungumzo kutaua suala hilo na kuzuia mzozo wa kijeshi kati yao, kama vile mamlaka ya Abbas huko Palestina na nchi za Kiarabu zinazozunguka hazichukui hatua za kijeshi dhidi ya umbile la Kiyahudi linayoikalia kimabavu na kuitaka Palestina! Kwa hivyo, Modi alianza na mpango wa kuziunganisha Jammu na Kashmir na kubadilisha demografia ya watu huko, na kisha kufuata uamuzi uliochukuliwa na Modi mnamo 5/8/2019 kufuta Kifungu cha 370 cha Katiba yao juu ya Kashmir...)

Amerika ilifikiri kwamba uunganushaji huo ungewafanya Waislamu kusahau kuhusu Kashmir na kwamba India na Pakistan zingekuwa bila matatizo kati yao, ikizingatiwa kwamba tawala hizo mbili kwa sasa zinafuata mstari wa Marekani. Amerika ilisahau, au ilijifanya kusahau, pamoja na India, kwamba Kashmir iko ndani ya nyoyo za Waislamu na itaregea, Mwenyezi Mungu akipenda.

c- Tatizo la kugawana maji na Pakistan. India ilitaka kuhakiki Mkataba wa Maji wa Indus uliopo. India kwa muda mrefu imekuwa ikitafuta kuhakiki Mkataba wa Maji wa Indus, uliotiwa saini mwaka 1960 na upatanishi wa Benki ya Dunia kufuatia miaka tisa ya mazungumzo, ikitoa sababu ya ongezeko la kasi la watu. Pakistan, hata hivyo, inakataa mazungumzo yoyote tena. Likinukuu vyanzo vya habari ambavyo havikutajwa jina, gazeti la “India Today” liliripoti kwamba: “India ilikuwa imesimamisha mtiririko wa maji kutoka Bwawa la Baglihar kwenye Mto Chenab hadi Pakistan.” Gazeti hilo lilionyesha kwamba India pia inapanga kukata mtiririko wa maji kutoka Bwawa la Kishanganga kwenye Mto Jhelum. (Shirika la Anadolu, 5/5/2025). Kwa kuzingatia usimamisha wa India wa mkataba huo uliohusisha upande mmoja na madai yake ya kudumu ya miaka mingi ya kuhakikiwa kwake, uamuzi wa serikali ya Modi kusimamisha mkataba huo baada ya shambulizi la Pahalgam unaweza kutafsiriwa kama jaribio la kuishinikiza Pakistan na kuilazimisha kukubali matakwa ya uhakiki. (“Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi imejaribu kujadili upya mkataba huo, na nchi hizo mbili zimejaribu kusuluhisha baadhi ya migogoro yao katika Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi jijini The Hague kuhusu ukubwa wa eneo la kuhifadhia maji katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kishanganga na Ratle.” (Arabi21, 27/4/2025).

Ni muhimu kufahamu kuwa Mkataba wa Maji wa Indus (ISA) ni mkataba wa ugawaji maji kati ya India na Pakistan. Ulitayarishwa na kujadiliwa chini ya udhamini wa Benki ya Dunia. Hafla ya kusainiwa kwa makubaliano haya muhimu ilifanyika Karachi mnamo 19/9/1960. Pakistan ilipewa haki ya kutumia maji ya mito mitatu katika sehemu ya magharibi ya Bonde la Indus (Jhelum, Chenab, na Mto Indus wenyewe), huku India ikidumisha udhibiti kamili wa maji ya mito mitatu ya mashariki (Sutlej, Beas, na Ravi).

c- Harakati za jihad huko Kashmir zilikuwa zikisababisha wasiwasi kwa India, kwa hivyo Amerika ilitaka kuzusha mapigano huko kama kisingizio cha shambulizi la India kwenye mizizi ya harakati hizo huko Kashmir na kujaribu kuhusisha serikali ya Pakistan katika shambulizi dhidi ya harakati hizo huko Pakistan. Hili lilifanyika katika hatua mbili:

Kwanza: Kuanzisha shambulizi huko Kashmir, kwa kulihusisha na harakati hizo, kwa kutumia kama uhalali wa operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya vituo vya harakati hizo nchini Pakistan, kama inavyodai ... na dhidi ya mizizi ya harakati hizo za Kashmir na dhidi ya Waislamu wa huko, kuwaua au kuwahamisha kwa kisingizio cha kuunga mkono harakati hizo, kama vile Mayahudi wanavyofanya huko Gaza kuuwa watu wake kwa kisingizio kuunga mkono upinzani. Halafu, iaibishe serikali ya Pakistan kwa kutoiunga mkono Kashmir kwa sababu shambulizi hilo lilianzishwa na harakati hizo!

Kwa hivyo, India ilianza, kwa amri ya Amerika kutekeleza shambulizi hili la uzushi huko Kashmir. Ushahidi wa hili ni:

- Shambulizi lililowalenga watalii katika Bonde la Baisaran katika eneo la Pahalgam la Kashmir inayotawaliwa na India mnamo tarehe 22/4/2025, ambalo India inadai lilitekelezwa na kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na Pakistan, huku Pakistan ikikanusha hilo. Shambulizi hili lilitokea Kashmir mnamo 22/4/2025, wakati Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance alikuwa jijini New Delhi. (Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance aliwasili India leo, Jumatatu, mwanzoni mwa ziara ya siku nne ambapo atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu Narendra Modi. (Shirika la Habari la Bahrain, 21/4/2025.) India ilichukua hatua zake zote za awali dhidi ya Pakistan, ikiwa ni pamoja na kusimamisha Mkataba wa Indus, wakati afisa huyu wa Marekani alipokuwa jijini New Delhi. Haya yanadhihirisha uratibu wa Amerika  na India, na haikubaliki kabisa kufikiri kwamba yote haya yalikuwa ni sadfa tu.

Haraka ya serikali ya India kuilaumu Pakistan kwa shambulizi la Aprili 22 dakika chache baada ya kutokea na kabla ya uchunguzi au utafiti wowote kuanza. Hii, ni licha ya matakwa ya Pakistan ya uchunguzi wa kimataifa, na vyombo vya habari vya India ambavyo vilifanya haraka kunyooshea kidole cha lawama TRF, mrengo wa Lashkar-e-Taiba (LET), licha ya kundi hilo kukataa kuhusika. Zote zinaonyesha operesheni "iliyopangwa". "TRF ilidai kuhusika na shambulizi hilo kwenye mitandao ya kijamii, lakini baadaye ilikanusha, ikitaja udukuzi kama kisingizio." (24.net, 30/4/2025)

Kisha awamu ya pili ilianza, huku India ikizindua mashambulizi ya makombora juu ya Pakistan jioni ya 6/5/2025. Haikujiwekea kikomo kwa sehemu ya Pakistan ya Kashmir, kama kawaida, lakini pia ililenga shabaha katika mkoa wa Punjab. Pakistan haikujibu kwa kulenga shabaha ndani ya India, lakini ilijiwekea mipaka kwenye mapigano ya mpaka na kuangushwa kwa ndege za India kwenye mpaka. India ilijaribu kupunguza athari za shambulizi hilo kwa Pakistan, ikisema kwamba haikushambulia shabaha za jeshi la Pakistan na ilishambulia tu "magaidi" (Al-Araby TV, 7/5/2025). Mapigano yaliendelea kuongezeka kati ya pande hizo mbili (mapigano makali yalizuka kando ya Mstari wa Udhibiti huko Kashmir kati ya vikosi vya India na Pakistan, na milipuko ilisikika kwenye Mstari wa Udhibiti (LoC) huko Kashmir huku kukiwa na ripoti za vifo, kulingana na vyombo vya habari vya India (Al-Arabiya, 9/5/2025). Ilikiri kwamba ndege zake 3 zilipigwa risasi katika Kashmir, na kutangaza kifo cha raia 7, na kutangaza vifo vya raia 7. Wakati Pakistan ikisema kwamba ilidungua ndege 5 za India, zikiwemo ndege tatu aina ya Rafale za Kifaransa, pamoja na droni 25 zilizotengenezwa na umbile la Kiyahudi, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alisema: ("Tungeweza kuangusha ndege 10 za kivita za India kujibu shambulizi la India kwenye maeneo ya Pakistan, lakini makamanda wa jeshi walijizuia na kuangusha ndege 5." 7/5/2025"). Msemaji wa jeshi la Pakistan Ahmed Sharif Chaudhry alitangaza kuwa jeshi lilishambulia kwa mabomu vituo 26 vya kijeshi na makumi ya droni zilizoruka juu ya miji mikubwa ya India, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, New Delhi (Sky News, 10/5/2025).  Inaonekana kwamba Pakistan ilikuwa na uwezo wa kuanzisha mashambulizi makubwa, kujihusisha katika makabiliano na India, na kuishinda. Lakini inafungamanishwa na Amerika, ambayo hairuhusu kufanya makabiliano kama hayo na kusababisha kushindwa kwa India, na kusababisha kuanguka kwa kibaraka wake Modi. Ingawa Amerika iliweza kushinikiza utawala wake kibaraka nchini Pakistan kuridhishwa na jibu dogo kwa uvamizi wa India, kile kilichoonekana kutokana na jibu hili dogo linaonyesha ushujaa wa askari wa Kiislamu nchini Pakistan na nguvu ya motisha yao ya kupigana. Licha ya njama za utawala wa Pakistan na Marekani na vizuizi vya harakati za jeshi, bado jeshi hili la Waislamu liliwaletea hasara kubwa maadui washirikina, kama tulivyotaja hapo awali. Haya yote yaliifanya Amerika kusitisha mpango wa vita ilipouanzisha, na kuamua kusitisha uvamizi iliouanzisha na kubadilisha mpango wa vita kuwa chuki ya kisiasa na mazungumzo kati ya tawala mbili zinazoitii, India na Pakistan. Hivyo kuifanikisha India na kile ambacho haikuweza kukifanikisha kupitia uvamizi wa kijeshi.

4- Kwa hivyo, siku nne baada ya kuanza kwa shambulizi la India, mnamo 10/5/2025, usitishaji wa mapigano ulitangazwa chini ya amri za Amerika. Rais Trump wa Marekani aliandika kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Kijamii (Truth Social) mnamo tarehe 10/5/2025, "Baada ya mazungumzo ya usiku mrefu yaliyoongozwa na Marekani, ninayofuraha kutangaza kwamba India na Pakistan zimekubaliana kusitisha mapigano kwa kina na mara moja. Napongeza nchi zote mbili kwa kutumia busara na akili ya juu. Asante kwa kuzingatia jambo hili." Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema kwenye jukwaa la X mnamo tarehe 10/5/2025, "Serikali za India na Pakistan zimekubaliana kusitisha mapigano mara moja na kuanza mazungumzo juu ya masuala mapana katika uwanja siyoegemea upande wowote." Aliongeza kuwa yeye na Makamu wa Rais J.D. Vance walifanya kazi na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar, Mkuu wa Majeshi ya Pakistan Asim Munir, na Washauri wa Usalama wa Kitaifa wa India na Pakistan Ajit Doval na Asim Malik katika siku mbili zilizopita kufikia makubaliano. Kwa maana nyengine, Amerika ilishindwa kuthamini ushujaa wa jeshi la Pakistan, licha ya utiifu wa uongozi wa jeshi hilo kwake, na waliogopa kwamba Modi angeendeleza mapigano hayo na kupoteza nguvu yake badala ya kutimiza matakwa ya Amerika katika kukabiliana na China! Kwa hiyo, iliamuru kusitishwa kwa vita hivyo na kukimbilia katika uovu wa kisiasa ili kufikia malengo yake kwa njia ya mazungumzo kati ya tawala mbili zilizotiifu kwake!

5- Kwa kumalizia, Hizb ut Tahrir inawatahadharisha Waislamu kwa jumla na watu wa Pakistan hasa kwamba uovu wa kisiasa na mazungumzo yanayofanyika na maadui wa Uislamu na Waislamu, hususan washirikina wa Kibaniani wa India na Mayahudi wa Palestina, mazungumzo haya hayaleti manufaa yoyote, hasa ikiwa mkoloni kafiri Marekani ndiye anayeyaendesha, kama inavyotokea sasa. Wanapigana vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kila wakati na kila mahali. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitufahamisha kupigana nao na kupata ushindi juu yao, na katika hayo yamo malipo makubwa. Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Ibn Umar kwamba Mtume (saw) amesema: «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...» “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawaua...” Ahmad na An-Nasa’i wamepokea kutoka kwa Thawban, mtumwa huru wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), aliyesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«عِصَابَتَانِ مِنْ أُمَّتِي أَحْرَزَهُمَا اللهُ مِنَ النَّارِ؛ عِصَابَةٌ تَغْزُو الْهِنْدَ، وَعِصَابَةٌ تَكُونُ مَعَ عِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ عَلَيْهِمَا السَّلَام»

“Kuna makundi mawili katika Ummah wangu ambao Mwenyezi Mungu atawakomboa na Moto: Kundi lenye kupigana na India, na kundi litakalokuwa pamoja na Isa bin Maryam, amani iwe juu yao wawili.”

Kwa hivyo, kupigana na Mayahudi huko Palestina na kuwaua, na kuivamia India na ushindi wa Uislamu ndani yazo bila shaka itatokea, Mwenyezi Mungu akipenda. Haya ni maneno ya Mkweli, Mwaminifu. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) amepitisha kwamba ushindi hautatushukia kutoka mbinguni, na Malaika wake watatubebea tukiwa tumekaa. Badala yake, tunahitaji kufanya kazi, kujitolea, na kujitahidi, na kutafuta haki na ikhalisi katika yale tunayofanya. Hivi ndivyo tunavyopaswa kuwa. Hapo, ndipo ushindi wa Mwenyezi Mungu utakuja, pasi na shaka, kwa idhini yake, utukufu ni wake.

Tuna matumaini makubwa juu ya watu wa Pakistan, kwani ni nchi yenye nguvu ya Kiislamu, na mizizi ya Uislamu imo ndani yake, na hisia za Uislamu zinazidi kuongezeka ndani yake. Jeshi lake linapenda jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na matarajio ya Waislamu huko  ya kusimamisha Khilafah yanazidi kuongezeka. Haitachukua muda mrefu, Mwenyezi Mungu akipenda, kabla ya kupatikana ushindi kwa kiongozi asiyewadanganya watu wake, na kauli yake (saw) itatimia kwa kusimamisha Khilafah Rashida baada ya utawala huu dhalimu tunaoishi ndani yake. Ahmad amesimulia katika Musnad yake kutoka kwa Hudhayfah ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَن تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَت...»

“Kisha kutakuwa na utawala wa kidhalimu na utakuwa muda anaoutaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauondoa Atakapotaka kuuondoa, kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza.” Na siku hiyo Waumini watafurahi.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

17 Dhul Qi’dah 1446 H

15/5/2025 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu