Alhamisi, 18 Dhu al-Hijjah 1447 | 2026/06/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  11 Dhu al-Hijjah 1447 Na: H 1447 / 085
M.  Alhamisi, 28 Mei 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ulaya Yahangaika Siku Chache Tu Bila Mafuta na Gesi ya Waislamu: Vipi Basi Ikiwa Ummah Ungeamka?!

(Imetafsiriwa)

Waziri wa Fedha wa Ufaransa Roland Lescure alisema kwamba serikali haziwezi kuamua kama zitoe akiba ya ziada ya mafuta ya kimkakati ili kupunguza usumbufu unaosababishwa na vita vya Iran hadi muda unaowezekana wa mzozo huo utakapokuwa wazi. Katika muktadha huo huo, mashambulizi ya awali ya makombora ya Iran kwenye kituo cha gesi cha Ras Laffan nchini Qatar, mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya gesi asilia vilivyoyeyushwa duniani, yalisababisha kupungua kwa kasi kwa akiba ya gesi ya Uingereza. Akiba ya gesi asilia nchini Uingereza ilishuka hadi viwango vya kutosha kukidhi matumizi ya ndani kwa muda usio zidi  masaa 48.

Kauli na matukio haya yanafichua uhalisia ambao kila mtu makini na mwenye ufahamu tayari anajua, lakini ambao watawala wa Magharibi na watawala wa ardhi za Waislamu wanatafuta kuuficha kwa hofu kwamba Ummah unaweza kutambua ukweli na kugeuza mambo kuwa chini juu.

Imekuwa dhahiri jinsi Magharibi ilivyo dhaifu na jinsi inavyotegemea Waislamu na rasilimali zao. Uingereza, dola yenye nguvu na ya kikoloni zaidi barani Ulaya, haikuweza kuhimili kukatizwa kwa usambazaji wa gesi wa Qatar kwa zaidi ya siku mbili, kana kwamba Qatar ilikuwa tangi la kuhifadhia gesi katika uwanja wa nyuma wa Uingereza kwa matumizi ya kila siku. Vivyo hivyo kwa Ufaransa, dola ya pili yenye nguvu zaidi barani Ulaya, ambayo maafisa wake wanazungumzia hitaji la haraka la kujua vita vitaisha lini ili kukadiria ni kiasi gani lazima kitolewe kutoka kwa akiba ya mafuta ya kimkakati. Wasiwasi kama huo miongoni mwa nchi zingine za Ulaya unaeleweka zaidi, kwani ziko katika hali dhaifu na hatarini zaidi. Mafuta na gesi ya Waislamu hutumika kama kawi ya kila siku ya dola za kikoloni za Magharibi.

Hii inathibitisha uhalisia mbili:

Kwanza: Ummah wa Kiislamu una bidhaa ya kimkakati ambayo, ikisimamiwa vizuri, inaweza kuuwezesha kuathiri nguzo muhimu za maisha ya kiuchumi katika Magharibi, zikiruhusu kuweka masharti, majukumu, na vigezo vya kuchagua, na hivyo kuwa katika mizani sawa badala ya kuwa chini.

Pili: Dola za kikoloni zinaishi kwa kutegemea utajiri na rasilimali za ardhi za Waislamu. Uti wa mgongo wa maisha yao ya kiuchumi unategemea kile kinachowafikia kutoka nchi za Kiislamu. Hii sio tu kwa mafuta na gesi, ingawa ni mifano maarufu zaidi. Pia inajumuisha madini, bidhaa za kilimo, kemikali, mbolea, na rasilimali zingine nyingi. Hii ni kweli hata kama rasilimali hizi zilinunuliwa kwa thamani yake ya haki. Vipi basi ikiwa tutatambua kwamba dola za kikoloni mara nyingi huzipata kwa bei ndogo kupitia mipango inayofanana na ruzuku na zawadi zaidi ya ubadilishanaji halisi wa kibiashara?

Hakika, Magharibi ni tete na dhaifu, inafanya kazi kama vimelea kwenye mwili wa Ummah wa Kiislamu. Dola zake zingekabiliwa na matatizo makubwa haraka lau njia za uhai zinazopanuka hadi ndani kabisa ya ulimwengu wa Kiislamu zingekatwa. Siku chache za vita tayari zimefichua uhalisia huu, kama vile zilivyofichua hadithi ya ngano ya nguvu ya kijeshi ya Magharibi isiyoshindwa.

Ummah wa Kiislamu unamiliki rasilimali, uwezo, na majeshi muhimu ili kujikomboa kutokana na utegemezi wa dola za kikoloni na hata kushindana nazo kwenye jukwaa la kimataifa. Kinachokosekana ni kiongozi mwenye ikhlasi anayesimamia mambo yake – Khalifa muongofu ambaye angetumia uwezo na rasilimali zake kuuregesha katika nafasi unayostahili katika kuongoza ulimwengu, kama ulivyokuwa hapo awali kwa karne nyingi. [وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ]  “Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.” [Surah As-Saffat:173]

Mhandisi Salah Eddine Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu