Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 2 Muharram 1448 | Na: H 1448 / 002 |
| M. Jumatano, 17 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ardhi Zetu Zitabaki Kukiukwa na Damu Yetu Itaendelea Kumwagika Hadi Tutakaposimamisha Khilafah Rashida Yetu
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumapili, tarehe 14 Juni 2026, jeshi la Kiyahudi lilifanya shambulizi la anga likilenga vitongoji vya kusini mwa Beirut, saa chache tu baada ya kuwaonya wakaazi wa takriban miji 30 kusini mwa Lebanon na kuwaamuru waondoke. Tovuti ya habari ya Axios iliripoti kwamba “jeshi la ‘Israel’ liliiarifu CENTCOM muda mfupi kabla ya shambulizi jijini Beirut kutokea.” Trump aliandika kwenye jukwaa lake la ‘Truth Social’ mnamo Jumapili: “Shambulizi la asubuhi ya leo dhidi ya Beirut halikupaswa kutokea, haswa katika siku maalum ambapo tuko karibu sana na Mkataba wa Amani na Iran.” Alisisitiza kwamba Marekani ilikuwa karibu sana kufikia makubaliano na Tehran na akasema kwamba “Hakupaswi kuwa na mashambulizi zaidi kutoka kwa Israel popote pale nchini Lebanon, lakini pia hakupaswi kuwa na mashambulizi zaidi kutoka kwa upande mwengine wowote, ikiwemo Hezbollah, dhidi ya Israel.” Wakati huo huo, hata hivyo, alisisitiza kwamba “Israel ina haki ya kujihami.”
Matukio na kauli hizi haziachi nafasi ya shaka kwamba umbile la Kiyahudi ni mradi muovu wa kikoloni ambao kwao upatanishi na upole haufai. Kwa idhini kutoka Amerika, mkuu wa ukafiri duniani, inaendelea kuteka kusini mwa Lebanon, kuwaua Waislamu kila siku, na kushambulia nyumba na majengo kwa mabomu. Shule wala hospitali hazijasazwa. Inahalalisha vitendo hivi kupitia imani inayowaweka wengine nje ya mipaka ya ulinzi.
[ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُواْ لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ]
“Haya ni kwa kuwa wakisema: Hatuna lawama kwa ajili ya hawa wasio jua kusoma. Na wanamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, hali nao wanajua.” [Surah Aal Imran :75]. Amerika na rais wake Trump wanaunga mkono suala hili. Maafisa wa Kiyahudi, akiwemo waziri wao mkuu, wamesema kwamba wanafurahia uungaji mkono wa Washington wa kulenga vitongoji vya kusini mwa Beirut endapo chama cha Iran nchini Lebanon kitashambulia vituo vya watu kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kimabavu.
Trump hajali, na hata anakaribisha, uvamizi wa Lebanon yote badala ya kusini mwake tu, na mauaji ya watu wake. Wasiwasi wake mkuu ni kwamba vitendo kama hivyo havipaswi kuingilia mazungumzo na Iran. Hii inaelezea utata katika kauli zake: kuelezea upinzani mdogo kwa ulipuaji wa mabomu katika vitongoji vya kusini mwa Beirut huku wakati huo huo akithibitisha “haki ya kujihami” ya umbile la Kiyahudi. Wakati huo huo, viongozi wa Kiyahudi wanatangaza wazi kwamba wana uungaji mkono kamili wa Marekani kwa vitendo vyao.
Kwa hivyo, ushirikiano wa Amerika na umbile la Kiyahudi unaendelea kutoa shinikizo kwa ardhi moja ya Kiislamu baada ya nyengine: Palestina, Syria, Lebanon, Yemen, Iraq, Afghanistan, na Iran. Orodha inaendelea, na hakuna anayejua ni nchi gani ijayo itakayolengwa - Misri na Uturuki, kama umbile la Kizayuni linavyopendekeza, au mtu mwengine? Maadamu ardhi za Kiislamu zitaendelea kugawanyika na kugawanywa, huku kila moja ikitawaliwa na mlinzi wa maslahi ya kikoloni, zote zinabaki kuwa katika hatari ya kuangamizwa na kutawaliwa.
Ulimwengu wa Kiislamu usingepata kamwe udhalilifu na udhaifu kama hiyo kama ungeunganishwa chini ya Khilafah moja na jeshi moja. Amerika na dola za kikoloni za Magharibi zisingeweza kutawala, wala umbile la Kiyahudi lisingekuwa na ushawishi wowote muhimu, sembuse uwezo wa kutenga na kulenga kila ardhi ya Kiislamu binafsi binafsi.
Nguvu ya Waislamu iko katika umoja wao, na heshima yao iko katika kutabikisha Uislamu, na wokovu wao uko katika kuregesha mamlaka yao na kumpa ahadi ya utiifu Khalifah Rashid (Khalifa muongofu) ambaye atawaunganisha tena, ataongoza majeshi yao katika vita vya ushindi na ukombozi, ataweka mipaka kwenye uvamizi wa Amerika na dola zote za kikoloni, na kulitokomeza umbile la Kiyahudi.
[وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.” [Surah Al-Munafiqun :8]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today |



