Mgogoro wa Kifedha: Thibitisho Jingine la Udhaifu wa Uchumi wa Kirasilimali
- Imepeperushwa katika Kenya
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hazina ya Taifa imekiri waziwazi kuwa Kenya kwa sasa inakumbwa na mgogoro wa kifedha. Waziri wa Fedha Henry Rotich amefafanua kuwa jumla wa mikopo ya ndani na ya kimataifa ambayo muda wake wa malipo umewadia imesababisha migogoro ya kifedha na mwendo wa kinyonga wa ukusanyaji ushuru umechangia pakubwa hali hii.