Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  2 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: H 1445 / 23
M.  Ijumaa, 10 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh iliandaa Kisimamo cha Kulaani Mauaji ya Halaiki Gaza
Enyi Waislamu! Kataeni ‘Suluhisho la Dola Mbili’ na Mutoe Wito kwa Maafisa wa Jeshi Wafuate Nyayo za Salahuddin Ayyubi ili Kuikomboa Palestina

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, leo, Ijumaa (10/5/2024), iliandaa visimamo na maandamano ya kulaani katika majengo mbalimbali ya misikiti ya Dhaka na Chittagong, yenye kichwa “Enyi Waislamu! Kataeni 'Suluhisho la Dola Mbili' na mutoe wito kwa maafisa wa jeshi kufuata nyayo za Salahuddin Ayyubi ili kuikomboa Palestina." Mwanzoni mwa Maandamano hayo, washiriki walionesha mabango mbalimbali, shamrashamra na kuimba kauli mbiu mbalimbali dhidi ya makruseda wa Kimagharibi, umbile la Kiyahudi na watawala wasaliti wa Waislamu na kwa ajili ya operesheni za kijeshi za kuikomboa Palestina kama vile: ‘Suluhisho la Dola Mbili’, Tiba ya Makafiri; Tumeni Majeshi ya Waislamu – Ikomboeni Palestina; Waislamu ni Mwili Mmoja; ‘Kwa nini ndege ya Israel iko Dhaka – Tunataka majibu; Israel ni kivuli cha watawala wasaliti wa Waislamu’; ‘Khilafah Pakee nidyo itakayoikomboa Palestina; 'La ilaha illallah - Al Khilafah Wada'Allah'.

Wazungumzaji katika mkutano huo walisema: Wakati mauaji dhidi ya Waislamu mjini Gaza, Ukingo wa Magharibi na maeneo mengine yakiendelea, serikali ya Hasina imechukua hatua ya kuhalalisha mahusiano na umbile haramu la Kiyahudi, sehemu yake ikiwa ni ndege mbili za mizigo kutoka "Israel" zilitua Bangladesh siku mbili mfululizo. Kama mnavyojua, serikali ya Hasina haijatuma vikosi vya kijeshi kuwalinda Wapalestina, lakini imetuma timu ya wanamaji 75 chini ya UN kwenda kwenye mpaka wa Lebanon kulinda umbile la Kiyahudi.

Wazungumzaji katika mkutano huo walitoa wito wa kukataliwa kwa 'Suluhisho la Dola Mbili': Watawala wasaliti wa Waislamu, akiwemo Hasina, wanachukua msimamo wa Marekani kuhusu Palestina, ambao kila mara huanza na wito wa kusitishwa mapigano na kumalizia kwa pendekezo la ‘Suluhisho la Dola Mbili’. ‘Suluhisho la Dola Mbili’ ni hatua ya mwisho katika njama dhidi ya Waislamu wa Palestina. Kama mnavyojua, mnamo 1917, ‘Tamko la Balfour’ la Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza lilijumuisha uungaji mkono wa serikali ya Uingereza kwa uanzishwaji wa makao ya kitaifa ya Mayahudi nchini Palestina. Tangu wakati huo, wakimbizi wa Kiyahudi waliofukuzwa kutoka nchi mbalimbali za Ulaya waliingia Palestina kwa makundi na kuanza kuishi. Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, wakimbizi wa Kiyahudi walimiminika Palestina kwa wingi na kuanza kuwafurusha Waislamu kutoka makwao. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, chini ya usimamizi wa Marekani, mnamo Novemba 1947, kwa mujibu wa Azimio 181 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Palestina iligawanywa na uvamizi huu haramu wa Mayahudi ulitambuliwa kama dola halali. Kwa msaada wa makruseda wa Kimagharibi ikiwemo Uingereza na Marekani, umbile hili haramu la Kiyahudi kwa sasa linakalia kimabavu karibu 85% ya ardhi ya Palestina. ‘Suluhisho la Dola Mbili’ linatambua uvamizi huu haramu wa ardhi ya Wapalestina. Zaidi ya hayo, dola hiyo iliyopendekezwa ya Palestina isiyo na nguvu ya kijeshi iliundwa kwa kuzingatia sera ya kuwapokonya silaha milele Waislamu wa Palestina ili kwamba umbile la Kiyahudi kamwe lisikabiliane na upinzani.

Kuhusu kufuata nyayo za Salah al-Din Ayyubi kuikomboa Palestina, wazungumzaji walisema: Mwenyezi Mungu (swt) anasema kuhusu watawala wanafiki,

[صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ]

“Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.” [Surah Al-Baqarah: 18]. Kwa hiyo, ni lazima tuwaelekee maafisa wa jeshi wanyoofu na kuwashajiisha watoto na ndugu zetu jeshini kwa ajili ya ukombozi wa Palestina; ili wafuate nyayo za Salahuddin Ayyubi. Ambaye aliwapindua watawala wanafiki na kuziunganisha ardhi za Waislamu na kufanya kampeni ya kijeshi ya kuikomboa Jerusalem kutoka mikononi mwa Wanajeshi wa Msalaba wa Kikristo mwaka 1187. Kikwazo kikubwa cha ukombozi wa Palestina ni utawala wa sasa, vibaraka wa Magharibi, ambao wanaliweka jeshi letu ndani ya kambi. Kwa hivyo, njia ya kweli ya kuikomboa Palestina ni kutoa wito kwa watoto na ndugu zetu katika vikosi vya kijeshi kuondoa matabaka haya tawala yanayozuia njia ya ukombozi wa Palestina na kutoa nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena utawala wa Khilafah, Dola ya Khilafah itaikomboa Palestina kupitia operesheni za kijeshi, insh'Allah.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu