Afisi ya Habari
Kenya
H. 15 Rabi' II 1446 | Na: H 1446/03 |
M. Ijumaa, 18 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut Tahrir / Kenya Yafanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki dhidi ya Watu wa Gaza
(Imetafsiriwa)
Kufuatia kuendelea kwa mauaji ya watu wa Gaza yanayofanywa na umbile katili la Kiyahudi ambayo sasa yamepita mwaka mmoja, Hizb ut Tahrir/Kenya kupitia Afisi yake ya Habari ilifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo siku ya Ijumaa, 18 Oktoba 2024. Mkutano huo na waandishi wa habari ulihudhuriwa na vyombo vya habari vinane nchini.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliochukua takriban dakika 20, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya, Ustadh Shabani Mwalimu alisisitiza mafunzo kadhaa ambayo Umma unapaswa kupata kutokana na mauaji yanayoendelea: maumbile ya ushujaa ya Waislamu huko Gaza, unafiki wa Baraza la Usalama na jumuiya nzima ya kimataifa miongoni mwa menngine yanayotolewa kutokana na mauaji hayo.
Hizb ut Tahrir / Kenya, ilikariri kuwa uvamizi wa kijeshi wa Wazayuni utaondolewa tu kwa ukombozi wa kijeshi. Na ukombozi wa Palestina kamwe hautakuja kupitia diplomasia au maazimio ya kimataifa. Majeshi ya Waislamu na watu wenye nguvu wana jukumu kubwa la kuwanusuru wana wa Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina. Hizb ilito wito kwa Ummah kufanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itawakomboa na kuwaunganisha Waislamu, na kuregesha uadilifu, usalama, na heshima kwa wanadamu wote.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/kenya/4276.html#sigProIdac0f8cca19
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |