Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  29 Sha'aban 1437 Na: 1437/03 H
M.  Jumapili, 05 Juni 2016

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ramadhani Inapasa Kutuwezesha Kupata Daraja ya Juu Kabisa ya uchaji Mungu

Kwa munasaba wa Mwezi wa Kheri wa Ramadhani, Chama cha Kisiasa cha Kiislamu Hizb ut Tahrir Kenya kina watakia Waislamu wote nchini Kenya na kote duniani kwa jumla Ramadhani Kareem na Saumu Maqbul. Hakika ni msimu wa furaha kuushuhudia Ummah wa Kiislamu wakiutukuza Mwezi huu na ni alama kuwa Ummah huu uko hai licha ya kupitia njama za kikatili za maadui wa Uislamu.

Tunawakumbusha Waislamu wanapokuwa wamefunga kuhakikisha wanafikia lengo lililotajwa na Mwenyezi Mungu (swt) ambalo ni uchaji Mungu.

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)

“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.” [TMQ 2:183].

Uchaji Mungu ni daraja ya juu kabisa kwa Muislamu inayomlazimisha kujifunga na Mwenyezi Mungu (swt).

Tunatoa wito kwa wale walio na uwezo miongoni mwa Waislamu kuwasaidia masikini miongoni mwa Waislamu kwa kuwapa sadaka na kufuturu nao. Kitendo hiki kinashajiishwa katika Uislamu na kiuhalisia umeweka sheria za kudhibiti umasikini. Kinyume na sera za mfumo wa kirasilimali za ubinafsi, ulafi na ukatili ambazo zimesababisha mwanya mkubwa kati ya tajiri na masikini. Mfumo huu umesababisha mizozo mingi sio tu katika upande wa kiuchumi bali pia kisiasa na kijamii.

Tunawasisitiza Waislamu kuisoma Qur'an kwa kutafakari maana iliyo ndani yake na pia kushikamana imara na mafundisho yake yanayo tokamana na Muumba wa wanadamu ambaye Mwenyezi Mungu (swt). Qur'an iliteremshwa katika Mwezi wa Ramadhani ili iwe ni uongofu kwa wanadamu katika kutatua matatizo yakiwemo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Lakini uongofu huo kwa karne kumi na tatu takribani nusu ya ulimwengu ulipata kiwango cha juu kabisa cha ufanisi katika sekta zote za maisha, kwani sheria za Qur'an zilitekelezwa kupitia Khilafah – utawala wa Kiislamu. 

Mwisho, tunasema ni muhimu mno kuwaombea dua sana Ndugu zetu Waislamu ambao kwa sasa wanakumbwa na hali mbaya na majanga katika nchi tofauti katika ulimwengu wa Waislamu. Hii ni kwa sababu dua ya mwenye kufunga hujibiwa kwa haraka. Tunajua kwa hakika kwamba mateso dhidi ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu yatakwisha pekee pindi tutakapo tekeleza mojawapo ya faradhi kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume katika mojawapo ya mataifa makubwa ya Waislamu. Khilafah ndio dola pekee ambayo itaung'oa urasilimali wa Kimarekani kupitia kuwafurusha maadui zake ambao wanaeneza ufisadi juu ya ardhi.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu