Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 6 Safar 1447 | Na: 1447/10 |
M. Alhamisi, 31 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Yeyote Anayezuia Mkate Usifike Gaza Hapaswi Kuzungumzia kuhusu Utu, Ewe Waziri wa Mambo ya Nje
Rafah: Imo ndani ya Tundu la Uvamizi... au imo Ndani Mshiko wa Serikali ya Misri?!
(Imetafsiriwa)
Katika mandhari ambayo hakuna jicho linaloweza kukosa kuiona, watoto wa Gaza wanasimama kwenye vifusi vya nyumba zao, wakikimbilia tama la maji, kipande cha mkate, au dozi ya dawa, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri anajitokeza mbele yetu akizungumzia "nia ovu" na "heshima ya sera ya kigeni," katika jaribio la kuiondolea serikali ya Misri dori yake halisi katika mzingiro wenye kunyonga pumzi uliolazimishwa juu ya Ukanda wa Gaza.
Waziri Badr Abdel Aati alisema katika mahojiano ya televisheni mnamo tarehe 30 Julai 2025 kwamba Misri inatekeleza sera yake ya kigeni kwa "heshima na utu," na kwamba "kivuko kiko wazi masaa 24 kwa siku," akidai kwamba mtu yeyote anayetilia shaka dori ya Misri ima ni mjinga au ana nia mbaya, akikashifu baadhi ya vyama na vikundi ambavyo alivitaja kuwa vya kigaidi vyenye kujaribu kuichafulia jina Misri, na kutoa wito hasira zielekezwe kwa uvamizi na sio Misri.
Lakini je, kauli kama hizo zinaweza kuwahadaa wale walioshuhudia mauaji hayo, wakahesabu malori yaliyokamatwa, na kuwaona majeruhi wakiomba kwa kusihi kwenye lango la kivuko cha Rafah?
Ingawa Waziri huyo anadai kuwa kivuko cha Rafah kinafunguliwa masaa 24 kwa siku, mashirika ya kimataifa, Umoja wa Mataifa, na Shirika la Msalaba Mwekundu yanathibitisha kwamba kimefungwa kwa siku nyingi tangu kuanza kwa uvamizi wa Mayahudi mnamo Oktoba 2023. Bora zaidi, kilifunguliwa chini ya masharti magumu ya usalama, na kupitia orodha za uratibu zilizoandaliwa katika afisi za asasi za usalama, ambazo makundi ya wahitaji zaidi yalitengwa.
Picha za satelaiti, ripoti za mashahidi, na timu za madaktari zimeonyesha kuwa kivuko kilibaki kimefungwa kwa masiku mfululizo, licha ya mrundikano wa mamia ya malori ya misaada upande wa Misri. Hili lilipelekea baadhi ya madereva kurekodi video zinazoonyesha kuharibika kwa dawa na vifo vya mifugo kutokana na ucheleweshaji huo. Hivyo uko wapi utu katika hilo ewe Waziri wa Mambo ya Nje?!
Waziri huyo anajaribu kuhalalisha kufeli katika kutoa msaada, kuwahamisha waliojeruhiwa, kushiriki katika mzingiro, na kushiriki katika mauaji hayo, kwa kusema kwamba "uvamizi uliharibu upande wa Palestina wa kivuko hicho." Lakini udanganyifu huu unapuuza ukweli kwamba mamia ya vivuko vya misaada ya kibinadamu duniani kote vilifunguliwa wakati wa vita vya kikatili zaidi, na uokoaji na utoaji wa misaada ulifanyika chini ya mabomu.
Kwa kweli, kile kinachoitwa upande wa Palestina wa kivuko cha Rafah ni afisi tu na vyumba vya usalama vilivyo upande wa pili wa lango la Misri. Kivuko cha muda cha dharura kinaweza kuundwa kwa urahisi, au korido kufunguliwa kando ya ukanda wa mpaka karibu na Kerem Abu Salem. Hivi ndivyo nchi nyingi hufanya ambazo zinathamini uhai wa majirani zao. Na juu ya yote, ni wajibu wa Misri na jeshi lake kuvunja ukuta mzima wa kizuizi, kuondoa mpaka kati ya Misri na Gaza, na kuwanusuru watu wake kikamilifu.
Kinachofanyika ni mzingiro usio wa haki, na kunyimwa mahitaji kwa watu wa Gaza. Ni uhalifu ambao tawala zinashiriki—zile zinazotukuza mipaka ya Sykes-Picot na kuzuia ufunguzi wa vivuko, iwe kwa kula njama au kwa ukimya. Mtume (saw) amesema: «فُكُّوا الْعَانِيَ وَأَطْعِمُوا الْجَائِعَ وَعُودُوا الْمَرِيضَ» “Wakomboeni mateka, walisheni wenye njaa, na watembeleeni wagonjwa.” Na amepokewa al-Tabarani kutoka kwa Abdullah bin Umar (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسْلِمُهُ» “Muslim ni ndugu yake hamdhulumu wala hamsalimishi.” Na ‘hamsalimishi’ maana yake ni: hamuachi kwa adui, wala hamnyimi msaada, wala hamfungii vivuko usoni mwake, wala hawatazami watoto wake wakifa na kutofanya lolote!
Ama kuhusu madai ya Waziri kwamba hasira zinapaswa kuelekezwa kwenye uvamizi pekee, huu ni mkanganyiko kati ya adui wa asili na adui msaidizi, kati ya muuaji na yule aliyemshikilia mhasiriwa ili amuue. Mzingiro huo unafanywa kwa mikono ya Waarabu, kwa kufunga kivuko cha Rafah, kulazimisha vibali, kuondoa misaada, na kukataa kuruhusu kuingia kwa mafuta na vifaa vya matibabu.
Waziri huyo anasema kuwa asilimia 70 ya misaada iliyoingia Gaza ilikuwa ya Misri, kana kwamba hii inahalalisha kufungwa kwa kivuko kwa maelfu ya wagonjwa. Hata kama asilimia hii ni ya kweli, haihalalishi ufunguzi wa kuchagua kwa kivuko hicho kwa kasi isiyolingana na maafa, wala haiwaondolei jukumu wale walioshiriki katika mzingiro, au kukaa kimya kuhusu mauaji, au kutia saini mikataba ya uratibu wa usalama pamoja na muuaji.
Zaidi ya hayo, misaada, ingawa ni muhimu, sio fadhila. Wajibu wa Kiislamu ni kupeleka jeshi kuwanusuru watu wa Gaza na kuikomboa ardhi yote iliyobarikiwa. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal: 72]. Kwa hiyo nusra sio mchango—ni faradhi ambayo haiondoki kwa sababu ya migogoro au bajeti.
Kuwatuhumu wale wanaopinga kufungwa kwa kivuko hicho au kwa kimya cha dola ya Misri kuhusiana na jinai za uvamizi wa ugaidi au nia ovu ni mbinu ya kizamani ya kimabavu, inayotumiwa na tawala dhalimu kila mara ukweli unapowafichua.
Kwa hiyo je, maelfu ya madaktari walioandamana kulaani kuzuiwa kuingia Gaza ni magaidi?! Je, watoto wa Gaza wanaotaka kufunguliwa kwa vivuko ni magaidi?! Je, wanazuoni na wahubiri waliosema kuwa mzingiro huo ni uhaini ni magaidi?!
Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri si chochote ila ni kifuniko cha kisiasa cha kujifungamanisha wazi na msimamo wa kimataifa, kimya juu ya jinai za uvamizi huo, na kushiriki moja kwa moja katika kufunga kivuko ambacho ni njia ya mwisho ya uhai wa Gaza. Ama kuhusu majaribio ya kuficha dori hii na kuzitia doa sauti huru—hayatanyamazisha vilio vya watoto chini ya vifusi, wala vilio vya waliojeruhiwa, wala machozi ya wajane.
Kivuko hicho kinaweza kufunguliwa kwa matingatinga—ikiwa ndugu hao wanaonekana kuwa kweli ni ndugu —na waya kuanguka ikiwa utu una thamani zaidi kuliko ubwana wa kirongo. Na Ummah unamjua nani anayeusaliti, anayeuunga mkono, anayefanya siasa kwa heshima, na anayeuua kwa jina la “utu.” Yeyote anayezuia maji kwa watu wa Gaza, na akazuia chakula na dawa, na kuwatelekeza kwa adui, ni mshirika katika uhalifu mbele ya Mwenyezi Mungu, bila kujali ni kiasi gani anajaribu kuficha uso wake kwa barakoa za uzalendo au heshima.
Milango ya Gaza iko wazi kwa majeshi kabla ya misaada. Vivuko vyake havihitaji malori zaidi ya vile vinavyohitaji magari ya kivita. Yule aliyekufa kwa njaa hatarudi—lakini yule aliyemsaliti bado anaweza kuokolewa ikiwa atachukua hatua kabla ya kuchelewa.
Amkeni, Enyi majeshi ya Ummah—na muanze kutoka Misri… kwani Gaza haisubiri kauli zaidi, bali vikosi vya wakombozi.
[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]
“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako” [An-Nisa: 75]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |