Kizungumkuti cha Syria: Kati ya Ukosefu wa Utambuzi na Tumaini la Kweli
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya miaka 14 ya vita na ukandamizaji, Syria inaonekana iko tayari kwa mabadiliko huku utawala wa Bashar al-Assad ukianguka na vikosi vya upinzani, vinavyoongozwa na Abu Mohammad al-Julani, vikichukua Damascus. Hata hivyo, matumaini ya mustakabali mzuri zaidi yanavurugwa na ushawishi mkubwa wa dola za nje kama vile Marekani na Uturuki, ambao zinaongoza njia ya Syria chini ya mifumo ya kisekula, inayoungwa mkono na Magharibi kama vile Azimio 2254 la Umoja wa Mataifa. Hili linazua maswali muhimu sana kuhusu iwapo tumaini la kweli linaweza kuwepo bila kukataa utawala wa kigeni na kuzipa kipaumbele kanuni za Kiislamu.