Jumatano, 07 Shawwal 1447 | 2026/03/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Sera ya Serikali ya Kisekula nchini Uturuki inayokula Njama Dhidi ya Mapinduzi ya Ash-Sham ndiyo Sababu ya Kulipuka kwa Kiota cha Mapinduzi katika Ukombozi

Kauli za maafisa nchini Uturuki kuhusiana na maridhiano na utawala uliopitiliza na kufunguliwa kwa mipaka kwa ajili ya maandalizi ya uhalalishaji mahusiano na utawala huo, na vitendo vinavyouandama vya ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wa Syria hasa wa Kayseri ni matokeo ya kimaumbile ya maneno ya uchochezi dhidi ya watu wa Syria, wakimbizi wanaoukimbia utawala wa Assad, na wanasiasa nchini Uturuki, wawe wenye mamlaka au wa upinzani, yote haya si lolote bali ni kuonyesha sura halisi ya utawala wa Uturuki, ambao unatekeleza mpango wa Marekani katika eneo hilo kufikia kile wanakiita suluhisho la kisiasa na kurudisha yale mabaki ya mji uliokombolewa kwenye kumbatio la utawala wa kihalifu.

Soma zaidi...

UNAMA Inashughulikiwa kwa Mapenzi huku Wabebaji Dawah Waislamu Wakijibiwa kwa Ukandamizaji?!

Mnamo Julai 9, 2024, Afisi ya Misheni ya Msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) ilichapisha ripoti ambayo utendakazi wa miaka 3 wa serikali ya Afghanistan kuhusu ‘haki za binadamu’ umekaguliwa. Katika ripoti hii ya kurasa 30, UNAMA imelaani na kukashifu vikali shughuli za Wizara ya Uamrishaji Mema na Ukatazaji Maovu, ikiviita vitendo vyake kuwa ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Soma zaidi...

Serikali ya Uzbekistan Inataka Kuwafunga Wafungwa 39 Wa Zamani wa Kisiasa kwa Miaka Mingi Zaidi

Enyi Waislamu wa Uzbekistan! Je, mnajua kwamba miongoni mwenu kuna vijana wachamungu na wenye ikhlasi ambao wamekaa miaka mingi ya maisha yao katika magereza, katika vyumba vilivyojaa unyevunyevu, katika hali ya kinyama iliyojaa shinikizo la kisaikolojia na kimwili, kwa sababu ya kusema kwao, “Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu”?!

Soma zaidi...

Mauaji ya Kikatili dhidi ya Watu Wetu mjini Gaza Bila Uwajibikaji! Lini Tutayaona Majeshi ya Waislamu Yakiinuka?!

Wizara ya Afya mjini Gaza imetangaza kuwa mashahidi 79 na majeruhi zaidi ya 289, baadhi yao wakiwa katika hali mahututi, wamewasili katika hospitali ya Nasser Medical Complex kufuatia mashambulizi ya mabomu kwa kambi za watu waliokimbia makaazi yao huko Mawasi Khan Yunis. Mauaji haya yanajiri baada ya uvamizi huo kufanya mauaji ya kutisha katika eneo la viwandani la kitongoji cha Tel al-Hawa, katika vitongoji vya Mji wa Gaza, na katika kambi za eneo la kati, na kusababisha zaidi ya mashahidi 100, na kuongeza kwa kasi idadi ya majeruhi.

Soma zaidi...

Marekani Inatafuta Ushindi Madhubuti nchini Afghanistan

Serikali ya Marekani, kupitia taasisi za kimataifa, hasa Umoja wa Mataifa, inalenga kupata ushindi madhubuti. Ni ushindi ambao haikuweza kuupata, licha ya zaidi ya miaka ishirini ya vita dhidi ya Uislamu na Mujahidina nchini Afghanistan. Utafutaji ushindi huu ulianza pale Marekani ilipoiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa vuguvugu la Taliban, na kufungua afisi kwa ajili ya vuguvugu hilo huko Doha mwaka 2013. Kupitia afisi hii, Marekani ilijihusisha kisiasa na harakati hiyo, na kusababisha duru kadhaa za mazungumzo yaliyohusisha Marekani na waamuzi, ukiwemo ujasusi wa Pakistan.

Soma zaidi...

Serikali ya Misri Inayakusanya Makundi ya Sudan kwa Manufaa ya Marekani na Kumakinisha Mamlaka yake, Sio kwa Manufaa ya Taifa au Watu wa Sudan!

Mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 6 Juni 2024, kongamano la vikosi vya kisiasa vya kiraia vya Sudan lilizinduliwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo, katika jaribio jipya la Misri kumaliza vita vinavyoendelea nchini Sudan. Waangalizi wanaamini kuwa jaribio hili linaweza kuweka msingi wa mazungumzo mapana, huku wengine wakipuuza umuhimu wa mafanikio ambayo linaweza kufikia. (Al-Araby Al-Jadeed).

Soma zaidi...

Mwito wa Mabadiliko: Uislamu Mfumo pekee Usiocheza Shere na Kuhujumu Maisha ya Watu

Kenya, imekumbwa na maandamano makubwa katika masiku ya hivi majuzi baada ya bunge kupitisha mswada wa kuongeza ushuru – ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kila siku kama vile mafuta ya kupikia, nepi, na mkate – kwa idadi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na mfumko wa bei na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira. Rais Ruto alikataa kutia saini mswada huo baada ya maandamano makubwa ambayo kufikia sasa watu 39 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu