Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 408
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 24 Agosti, tume inayoitwa "Tume ya mapambano ya wanawake yaliyosahaulika" iliyopewa kazi na serikali ya Denmark, ilichapisha mambo tisa ya kupambana na kile ambacho kimeanzishwa katika siasa za Denmark kama "udhibiti hasi wa kijamii". Pendekezo, lililopata mjadala mkali zaidi katika vyombo vya habari vya Denmark na kwenye mitandao ya kijamii, lilikuwa ni pendekezo la kupiga marufuku hijab za Kiislamu katika shule za msingi.
Mnamo Jumanne, tarehe 30/8/2022, ujumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Tunisia, ukiongozwa na Ustadh Yassin Bin Yahia, wakiwemo wajumbe Ustadh Al-Habib El Madini na Mohammad Ali Bin Salim, walitembelea Taasisi ya Tunisia ya Mafunzo ya Kimkakati, ambayo ni taasisi rasmi chini ya usimamizi wa Afisi ya Rais wa Jamhuri.
Qur'ani Tukufu ni Kitabu cha Mola wetu Mlezi aliyekiteremsha kwa lugha ya Kiarabu. Mwenyezi Mungu (swt) amewapa furaha wanadamu wote, kupitia kushikamana na mwongozo Wake na kufuata Njia Yake. Yeye (swt) ametahadharisha kila aina ya dhiki kwa yule inayemsibu na kujiepusha na njia hiyo.
Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alitangaza nia ya Moscow ya kuimarisha kambi za kijeshi nchini Tajikistan na Kyrgyzstan kuhusiana na hali nchini Afghanistan. Mkuu huyo wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi alitoa taarifa hiyo dhidi ya mazingira ya mazoezi ya kijeshi nchini Tajikistan "Ushirikiano wa Kikanda - 2022" pamoja na ushiriki wa nchi za Asia ya Kati, Amerika, Mongolia na Pakistan.
Mafuriko ya hivi karibuni nchini Pakistan sio tu yamesababisha uharibifu lakini ukubwa wa maafa umepita mafuriko ya awali ya 2010 na tetemeko la ardhi mwaka 2004. Zaidi ya theluthi moja ya nchi iko chini ya maji na zaidi ya watu milioni 33 wamekimbia makaazi yao.
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, aliandika kwenye anwani yake rasmi ya Twitter mnamo 8 Septemba 2022, “Nimehuzunishwa sana na kifo cha Mtukufu Malkia Elizabeth II. Pakistan inaungana na Uingereza na mataifa mengine ya Jumuiya ya Madola kuomboleza kifo chake.”
Mnamo Jumapili, Amri Kuu ya Kijeshi ya Marekani (CENTCOM) ilitangaza kuanzisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi nchini Jordan, ikisisitiza kujitolea kwa Washington kwa washirika wake katika Mashariki ya Kati kwa ulinzi wa pamoja dhidi ya matishio mbalimbali.
Mamlaka ya Udhibiti wa Soko la Nishati la Uturuki (EPDK) ilitangaza ongezeko la ushuru wa umeme kwa vikundi vya utumizi wa nyumbani kwa 20%, na kwa vikundi vya utumizi wa viwanda kwa 50%.
Kiwango cha nguvu za kisiri za Malkia na Mwanamfalme Charles za kura ya turufu juu ya sheria mpya kimefichuliwa baada ya Downing Street kushindwa kuweka taarifa kuhusu matumizi wake kuwa siri.