Jumanne, 06 Shawwal 1447 | 2026/03/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ushirikiano wa Mamlaka za Uholanzi pamoja na Watu Ovyo wa Mayahudi Umesalia Kuvama ndani ya Kumbukumbu ya Umma

Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti vitendo vya kundi la wachochezi wa Kiyahudi wakati na baada ya mechi ya kandanda, kujihusisha na uchokozi dhidi ya Waislamu kuhusiana na kadhia kuu ya Umma wa Kiislamu, kadhia ya Palestina. Vitendo hivi viliibua hisia za kimaumbile kutoka kwa Waislamu wa mataifa mbalimbali na kutoka kwa raia waheshimiwa wa Uholanzi wenyewe.

Soma zaidi...

Mkutano wa kilele wa Riyadh: Ushahidi kwa Usaliti wa Viongozi wa Waislamu dhidi ya Gaza na Lebanon

Zaidi ya siku 400 baada ya vita vya mauaji ya halaiki vilivyoanzishwa na umbile nyakuzi, halifu la Kiyahudi dhidi ya watu wetu huko Gaza, vita ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia, na kufuatia mauaji na uharibifu uliofuata nchini Lebanon, viongozi wa Waislamu walikutana jijini Riyadh kwa kile walichokiita kuwa ni “mkutano wa ajabu.” Matokeo, hata hivyo, hayakuwa chochote ila mfululizo wa maamuzi dhaifu ambayo yanaweza tu kusifiwa kuwa ya khiyana.

Soma zaidi...

Wito wa Kushiriki katika Chaguzi za Kimagharibi ni Wito wa Kujioanisha ndani ya Mujtamaa za Kikafiri za Kimagharibi, na Kuzuia Ulinganizi wa Ujumbe wa Uislamu kwa Ulimwengu Mzima

Katika kila uchaguzi unaofanyika katika nchi za Magharibi, iwe ni uchaguzi wa urais au ubunge, wanaharakati wengi katika jamii za Kiislamu katika nchi za Magharibi hupaza sauti zao wakitaka kushiriki katika chaguzi za ndani katika nchi hizo. Wanaharakati hao wakiwemo masheikh na maafisa wa vituo vya Kiislamu wanafanya kile kinachofanana na kampeni za uchaguzi wakiitaka jamii kukipigia kura chama au mgombea fulani. Hawatoi wito wa kuacha kupiga kura, hata kama wagombea hawapendi “masheikh” hawa, wakisisitiza ulazima wa kushiriki katika uchaguzi, na kupiga kura, hata kama mpiga kura Muislamu hatajaza chochote katika karatasi yake ya kupigia kura.

Soma zaidi...

IMF Kusifia Uchumi wa Tanzania ni Kuficha Uovu wa Shirika hilo

Kauli ya karibuni ya Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kwa Afrika bwana Willie Nakunyanda aliyoitoa Washington DC katika makao makuu ya IMF kwa ujumbe wa Tanzania, kwa kusifia, kupongeza na kuurembaremba uchumi wa Tanzania si chochote zaidi ya kebehi na dharau kwa Tanzania, wananchi wake na watu wa nchi changa kwa ujumla. Kauli hiyo inalenga kuficha nyuma ya pazia lengo baya, la kikoloni na la dhulma la taasisi za IMF na Benki ya Dunia (Bretton Woods Institutions).

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Tanzania Yatoa Wito kwa Majeshi ya Waislamu Kuiokoa Gaza

Kufuatia kampeni ya zaidi ya mwaka ya mkaliaji kimabavu umbile la Kiyahudi, ushenzi na dhulma kwa Waislamu wa Gaza na ardhi jirani za Waislamu zinafanywa kwa msaada wa Marekani, na mataifa mengine ya Kimagharibi na ushirikiano wa vibaraka katika ardhi za Waislamu.Hizb ut Tahrir / Tanzania ilifanya visimamo baada ya swala ya Ijumaa katika sehemu mbalimbali kupinga ukatili wa umbile la Kiyahudi na kutoa wito kwa majeshi ya Waislamu hususan Misri, Jordan, Syria, Uturuki, Saudi Arabia nk, kusonga mara moja ili kuwaokoa Waislamu wa Gaza.

Soma zaidi...

Je, Jamii ya Waislamu ina Dori katika Kuamua Uchaguzi wa Marekani?

Katika mkesha wa uchaguzi wa urais wa Marekani, Waislamu milioni 2.5 waliojiandikisha kupiga kura wanauliza jinsi gani wanaweza kuleta mabadiliko. Hawakubaliani kuhusu jinsi tofauti hiyo inavyofanyika, lakini kheri katika nyoyo zao inawaunganisha katika hamu yao ya kuona mauaji na maangamizi nchini Palestina na Lebanon yanafikia mwisho kwa namna fulani.

Soma zaidi...

Mvunjifu na Mdhamini Pamoja: Serikali Yalenga Nini?

Iwe ni serikali au upinzani, miundo kama hii ya kisiasa haiwezi kukwepa kuwa wafungwa wa ukoloni, kama vile mtazamo wao wakati wa Mapinduzi ya Kiarabu na Kimbunga cha Al-Aqsa kinachoendelea, wanatumikia maslahi ya makafiri wakoloni ili tu kudumisha viti vyao. Madhumuni yao pekee ni kuzuia ummah wa Kiislamu kuelekea katika Khilafah na kujaribu kuzalisha miungano bandia, dhidi ya umoja halisi wa Khilafah.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu