Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 7 Ramadan 1445 | Na: HTS 1445 / 26 |
M. Jumapili, 17 Machi 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ufunguzi wa Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan mjini Port Sudan
(Imetafsiriwa)
Kwa msaada na muongozo wa Mwenyezi Mungu, leo, Jumapili, tarehe 7 Ramadhan 1445 H, sawia na tarehe 17 Machi, 2024, Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan imezinduliwa mjini Port Sudan (mtaa wa Al-Athmah), kusini-mashariki mwa uwanja. Itatumika kama nguzo ya kueneza fikra za Kiislamu, jukwaa la thaqafa ya Kiislamu, kitovu cha utambuzi wa kisiasa, na nukta kianzilishi cha ubebaji ulinganizi kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya utume. Khilafah hii ndio alama ya kipekee katika safari ya Ummah, kwani inakabiliana na njia panda iliyolemewa na mizigo mizito, iliyolemewa na majeraha yaliyodumu kwa zaidi ya karne moja chini ya utawala wa serikali za kitaifa, zao la ukafiri wa kikoloni ambao ulipotosha imani, uliopuuzwa hukmu za Kiislamu, ulikiuka matukufu ya Waislamu na raia wa dola, na kusababisha mito ya umwagaji damu wa Waislamu, kupotea kwa usalama, na kuenea kwa umaskini, dhulma na unyang'anyi. Kinachotisha zaidi ni kwamba Ummah wetu unaingia kwenye njia panda hii, na nguvu za giza zinasisitiza kutuongoza katika njia ile ile, kwenye shimo refu—shimo ambalo tumeumwa mara kwa mara.
Ni wajibu kwetu sisi Waislamu katika mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, msimu wa kuregea kwa Mwenyezi Mungu, kusahihisha mwenendo wa maisha yetu yote na kukuza hatua za kuelekea kwenye alama ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Ufunguzi wa Afisi ya Hizb unalenga kuwafahamisha watu mradi wa Khilafah katika mifumo ya utawala, uchumi, masuala ya kijamii, sera ya elimu, na sera za kigeni. Tunasubiri kwa hamu ziara zenu za heshima. Kufanya kazi kuelekea kusimamisha Khilafah ni wajibu kwa Waislamu wote. Kupitia kwayo zitarekebishwa hali za watu wote, kwa kutimiza ahadi ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliyetakasika:
[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi” [Surat An-Nur: 55]. Na Mtume Muhammad (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://www.hizbuttahrir.today/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/3841.html#sigProId4150278f48
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |