Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  13 Rabi' I 1443 Na: 01 / 1443 H
M.  Jumatano, 20 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji ya Ariha ni Moja ya Msururu wa Vipindi vya Kuwanyenyekesha Watu wa Ash-Sham


(Imetafsiriwa)

Leo, Jumatano, tarehe 20/10/2021, raia wasiopungua 10 wameuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, wakiwemo watoto, kutokana na mashambulizi ya mizinga yaliyofanywa na dhalimu wa Ash-Sham kwenye mji wa Ariha viungani mwa Idlib, iliyoko ndani ya eneo la upunguzaji kasi ya vita kaskazini mwa nchi.

Enyi Waislamu wa ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Mauaji mapya yanafanywa mbele ya macho na masikio ya walimwengu, kana kwamba hakuna kilichotokea. Hii ni kwa sababu kila mtu anahusika katika jinai hii inayolenga kuyabatilisha mapinduzi ya Ash-Sham kwa kuvunja matakwa ya watu wake na kuwaweka chini ya suluhisho la kisiasa la Amerika.

Mauaji ya kinyama yaliyofanywa siku mbili tu baada ya mkutano wa Kamati ya Katiba, ambayo inashughulikia kutunga katiba inayodhamini umbile la kisekula la dola hii na inaziondoa hukmu za Uislamu kutoka kwa dola na serikali.

Kamati ya katiba ilichukua jukumu la kutoa cheti cha kifo kwa mapinduzi, na kuomboleza kujitolea muhanga kwa watu wake kwa jina la katiba ambayo ibara zake zinaundwa na zana za Magharibi na wapambe wake.

Mauaji yanayotangaza waziwazi kwa watu wote kwamba damu ya watu wa Ash-Sham imekuwa duni, baada ya watu wa Ash-Sham kudhibitiwa na watawala watumwa, watiifu, wasio huru katika kufanya maamuzi, walioporwa matakwa na hutekeleza maagizo ya mabwana wao kwao, na wanasimama pasi na kuchukua hatua mbele ya madhari iliyojaa na damu na viungo vya mwili.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, zizi la Uislamu:

Kujitolea muhanga mulikojitolea ni kukubwa na kiwango cha mateso muliyoyavumilia ni makubwa, kwa hivyo msiruhusu kikundi cha viongozi chenye uhusiano kwengineko kuchezea hatima yenu au kufanya biashara na kujitolea muhanga kwenu, kwani yeyote aliyemuasi dhalimu wa Ash-Sham ana uwezo wa kuwaasi madhalimu waliosalia mpaka afikie thamani ya mihanga yake, na hakuna kinacholipa kujitolea huku isipokuwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; ambayo kwayo viumbe ardhini na mbinguni vitatosheka, na kisha damu zote za Waislamu zitalipiwa kisasi, na madhalimu watasahau na minong’ono ya Shetani.

 [وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [As-Shu’ara: 227]

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu