Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  14 Rabi' I 1443 Na: 02 / 1443 H
M.  Alhamisi, 21 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kamati ya Katiba ni Chombo cha Magharibi katika Kuchora Mustakbali wa Watu wa Ash-Sham na Kuamua Umbo la Maisha yao.

 
(Imetafsiriwa)

Awamu ya sita ya kikao cha Kamati ya Katiba, ikiwa na sehemu zake mbili, mwakilishi wa serikali ya kihalifu na mwakilishi wa ule unaoitwa upinzani, ilianza Jumatatu, 18 Oktoba 2021, huu ni mkutano wa sita baada ya mikutano mitano kufeli.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham: Hapana shaka kwamba kazi ya kamati hii inategemea usaidizi wa jumuiya ya kimataifa na inafungamana nayo. Kwa hiyo, ibara zote zitakuwa chini ya idhini ya Kafiri Magharibi kwanza kabisa. Kitu kingine chochote kama vile dai la itifaki au kura ya maoni...nk si chochote ila ni dhihaka na danganya toto.

Katiba yoyote inayosimamiwa na Kafiri Magharibi bila shaka ni katiba inayoendeleza uvamizi, kwa sababu itaegemezwa juu ya mtazamo wake kwa msingi wa kutenganisha Uislamu na maisha na jamii, na hii ina maana ya kuingiza usekula katika serikali ambayo Kafiri Magharibi kwa muda mrefu imeusisitizwa katika makongamano yake kuhusu suala la Syria, na bila shaka yatachakachuliwa kulingana nayo katika ibara zake zote; kufikia maslahi yake kwa gharama ya maslahi ya watu wa Ash-Sham, kwa sababu Kafiri Magharibi inazichukulia nchi za Kiislamu kuwa makoloni yake, na imeweka vibaraka wake kwenye shingo za watu wao. Ikawaweka juu ya viti vya utawala ili kulinda maslahi yake, na kwa hiyo taabu na ugumu wa maisha ni vitu vilivyomo ndani ya katiba hizi zilizotungwa na mwanadamu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:  

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 124]. Kuifanya akili kuwa mtunzi sheria badala ya Mwenyezi Mungu, bila shaka, ni kukengeuka kutokana na Sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali ni kushindana na Mwenyezi Mungu katika Ufalme Wake.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, zizi la Uislamu: Mwenyezi Mungu Mtukufu amewausia Waislamu kuhukumu kwa sheria yake ya Haki (Shara'), ametakasika yule aliyesema:

]وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَنْ يُصِيبَهُمْ بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيراً مِنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.” [Al-Ma’ida: 49].

Ameifanya furaha na maisha ya starehe kuhusiana na kiwango cha kujitolea kwa Waislamu kwa sheria ya Mola wao Mlezi na mwongozo Wake; Amesema aliyetukuka:

 [فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى]

“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” [Ta-Ha: 123].

Kwa hiyo, mnapofanya mapinduzi dhidi ya dhalimu wa Ash-Sham; kuvikeni taji kujitolea muhanga kwenu kukubwa kwa kusimamisha faradhi ya Mola wenu Mlezi, bali taji la faradhi zake; na hiyo ni kwa kupitia kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, kwani Wallahi ndio furaha yenu duniani na Akhera, na bila shaka ndio heshima ya Waislamu, tamkini ya dini na radhi na rehema za Mola Mlezi wa walimwengu wote. Hili linadhihirishwa kivitendo kupitia kutabanni mradi wa wazi wa kisiasa unaotokana na Aqeedah ya Muislamu, na kutabanni uongozi wa kisiasa unaozingatia wenye ikhlasi na kujali ambao utawaongoza watu wa Ash-Sham kwenye usalama. Hapa lazima tuwakumbushe Waislamu kwa jumla na watu wa Ash-Sham haswa; kwamba sisi katika Hizb ut Tahrir tunawasilisha kwa Waislamu wote katiba ya Kiislamu iliyobainishwa katika vifungu vyake vyote kutoka katika Qur'an na Sunnah, na yale yanatuongoza kutokana katika Ijmaa ya Maswahaba na Qiyas ya Kisheria, ambayo yanayoonyesha sura ya dola ambayo Sharia yetu imetufafanulia, na kutuwekea taasisi zake na mamlaka ya lazima ya taasisi hizi, ili kile tunachotafuta kisibaki kuwa ni kauli mbiu tu, au matakwa jumla badala yake, lengo makhsusi ambalo tunalitafuta kwa utambuzi njia halali iliyonyooka.

Tunafanya kazi usiku na mchana pamoja na Ummah wetu, msingi wetu, na wale wanaotuunga mkono; hadi katiba hii itekelezwe katika dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume ambayo Mtume (saw) alitupa bishara yake njema pale aliposema:  «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha (saw) akanyamaza”.

Ahmad Abdul Wahhab

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu