Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 24 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: 1446/14 |
M. Ijumaa, 20 Juni 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Mabrouk Ben Nasser
[وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوفْ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الأَمَوَالِ وَالأنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ]
“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri” [Al-Baqara 2:155]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inaomboleza kwa huzuni na majonzi makubwa kuondokewa na ndugu yetu Mabrouk Ben Nasser, aliyefariki siku ya Alhamisi, 23 Dhu al-Hijjah, 1446 H, sawia na 19 Juni 2025 M. Alikuwa mmoja wa Mashababu (wanachama) wa Hizb ut Tahrir ambao walifanya kazi ndani ya safu zake wakati wa nyakati za giza za dhulma na ukandamizaji, akiwa amezuiliwa kwenye jela za Bourguiba na kisha Ben Ali. Alitumia muda wake kwa subira na imani, akiendelea kushikamana na ulinganizi wake na kujitolea kuubeba, akilingania Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Alisimama imara katika wito wake, akiiamini ahadi ya Mola wake Mlezi, na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw) mpaka kufa kwake. Hivi ndivyo tunavyomtazama, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie ndugu yetu Mabrouk bin Nasser daraja ya juu kabisa ya Pepo, na amjumuishe pamoja na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, wakiwemo manabii, wakweli, mashahidi na watu wema. Hao ndio marafiki wazuri walioje!
[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara 2:156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |