Jumamosi, 04 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/05/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  25 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: HTY- 1446 / 21
M.  Ijumaa, 23 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wananchi Wanataka Kupinduliwa kwa Serikali na Kusimamishwa kwa Utawala wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Aden, mji mkuu wa muda wa serikali ya Yemen, umeshuhudia maandamano matatu ya wanawake na wanaume katika wiki mbili zilizopita. Kutokana na mateso yanayoendelea kwa wananchi, maandamano ya hasira yamefanyika mjini Aden, wakidai huduma za msingi na kukemea hali ngumu ya maisha na huduma duni. Maandamano haya yalijumuisha kauli mbiu dhidi ya muungano wa Waarabu, serikali ya Yemeni, na Baraza la Mpito, ambalo linadhibiti mji mkuu wa muda, Aden. Maandamano haya pia yalishuhudia milio ya risasi na kukamatwa kwa baadhi ya waandamanaji. Maandamano haya yalifanywa na wanawake na wanaume kwa siku tofauti. Kilichotia fora ni kuregea kauli mbiu isemayo “Wananchi wanataka kupinduliwa kwa serikali,” ambayo inatukumbusha Mapinduzi ya Kiarabu dhidi ya ukandamizaji na udhalimu.

Sababu za mapinduzi dhidi ya utawala wa sasa wa Yemen ni kubwa kuliko sababu za mapinduzi ya 2011. Hali ya maisha ni mbaya zaidi, dhulma na umwagaji damu vinaendelea, na hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu inasalia kusitishwa. Ilikuwa ni jambo la kimaumbile kwa watu kutambua kwamba utawala haujabadilika, kwamba mfumo wa kijamhuri wa kisekula ungalipo, na kwamba lazima turudi kiweli kwenye wazo kwamba watu wanataka kuiangusha serikali. Hata hivyo, wakati huu lazima kuwe na mradi badali wenye mafanikio na ukweli ili juhudi na damu zisipotee bure, na mapinduzi yasigeuzwe na kutumiwa na vibaraka wachache wa Kafiri Magharibi, ambayo imesababisha uhalisia huu mbaya sana.

Kwa hiyo, ni lazima tueleze ni kwa nini Mapinduzi ya Kiarabu yaliyoanza mwaka 2011 hayakubadilisha hali za watu, bali zilizidi kuwa mbaya zaidi. Sababu muhimu zaidi ni kwamba, Kafiri Magharibi, kupitia vibaraka wake, waliyateka nyara mapinduzi, wakapotosha mkondo wake, wakafanya kazi ya kuwatenga watu wenye ikhlasi na wenye ufahamu, na kuzirudisha tawala ambazo watu waliziasi kupitia mlango wa nyuma, lakini kwa sura mbaya zaidi na ya kihalifu zaidi, ili kufikia malengo mawili: la kwanza: kuendelea kudhibiti nchi za Kiislamu kwa kuendelea kuutenga Uislamu kutokana na uhalisia wa maisha, na pili kuwafanya watu wapinge wazo la kufanya kazi kwa ajili ya mabadiliko na hata wajisalimishe kwa hali halisi ilivyo. Hali mbaya zaidi baada ya mapinduzi ni adhabu kwa watu kwa kuasi dhidi ya vibaraka wa Magharibi. Leo, mandhari katika nchi ambazo watu waliasi dhidi ya dhulma na giza haijatulia, kwa sababu ufahamu wa watu umeongezeka, na kufanya udanganyifu wa makafiri na mipango yao kuwa ngumu. Suluhisho ni kwa Waislamu kukusanyika katika Dini yao, kwani ndio njia pekee ya wao kupata ubora hapa duniani na kesho Akhera. Kukusanyika huku lazima kuwe nyuma ya uongozi na kambi inayofanya kazi kwa ajili ya Uislamu, isiyofungamana na Mashariki au Magharibi, bali yenye kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na kuwepo miongoni mwenu na pamoja nanyi. Nayo ni Hizb ut Tahrir.

Baada ya kuporomoka kwa Khilafah Uthmani, Waislamu nchini Yemen waliishi chini ya mifumo mbalimbali iliyobuniwa na mwanadamu. Walijaribu mifumo mbalimbali na hawakupata chochote zaidi ya taabu, uharibifu, mauaji, na uporaji, iwe ujamaa au ubepari, ambao ulimwengu wa leo unabeba mzigo wake. Uislamu pekee ndio ulio na suluhisho msingi la matatizo yote ya mwanadamu kupitia tiba za kweli kwa nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), Muumba. Waislamu na wengine wameishi chini ya uadilifu wake kwa amani na utulivu kwa karne nyingi. Je, tunatambua leo kwamba utatuzi wa matatizo yetu upo katika hukmu za Uislamu? Je, tunatambua kwamba hukmu hizi zinadhibiti ugavi wa mali, kudhibiti aina za mali, na kudhibiti njia ya kuwahisabu watawala iwapo watafanya dhulma au makosa? Je, Waislamu hawatambui kwamba Dini yao imefanya kuwahisabu watawala moja ya aina kuu za jihad? Imewadhaminia haki ya kutoa maoni yao na kukemea mapungufu yao, na imewahakikishia mahitaji ya msingi ambayo serikali inapaswa kuwapa, na kuwawajibisha wale wanaoshindwa kuyatimiza? Uislamu haujaacha jambo lolote dogo wala kubwa bila ya kuliwekea hukmu ya kisheria, na hakuna tatizo la kibinadamu bila kulipatia ufumbuzi sahihi. Kwa bahati mbaya, hukmu hizi zimefichwa kwa Waislamu, na kuwaacha wakiteseka chini ya ukandamizaji wa mifumo dhalimu ya kikafiri, wakiipoteza dunia hii na Akhera.

Enyi watu wenye imani na hekima: Hizb ut Tahrir inakulinganieni na kuwahimiza kufanya kazi kwa umakini na ikhlasi ili kuzipindua tawala hizi na kusimamisha utawala wa Uislamu kwenye magofu yao. Kwa ajili hiyo, imetayarisha katiba yenye ibara na sheria zinazotokana na hukmu za Dini yenu zinazoshughulikia matatizo ya maisha ili mupate furaha duniani na Akhera. Hatusemi haya kwa ndoto tu, bali tunafanya kazi miongoni mwa Ummah. Tumetayarisha njia ya kina inayotokana na sheria ya Mola wetu Mlezi. Zaidi ya yote, tunaamini ahadi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na tumehakikishiwa kwamba Mwenyezi Mungu atainusuru Dini yake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizbuttahrir.today
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu