Jumamosi, 18 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  10 Dhu al-Hijjah 1446 Na: HTY- 1446 / 23
M.  Ijumaa, 06 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Wilayah Yemen Inawapongeza Watu wa Imani na Hekima na Umma wa Kiislamu kwa Sikukuu ya Idd al-Adha iliyobarikiwa
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Yemen inatoa pongezi zake za dhati na baraka zenye thamani kubwa zaidi kwa watu wa imani na hekima, na kwa Amiri wa Hizb, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, na kwa wanachama wote wa Hizb, na kwa Ummah mzima wa Kiislamu kwa sikukuu ya Idd al-Adha iliyobarikiwa mwaka huu wa 1446 H. Mwenyezi Mungu airudishe kwao, juu yetu, na juu ya ulimwengu wote kwa kheri, baraka, na furaha.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu zote, auunganishe Umma wa Kiislamu baada ya kuchanika na kugawanyika, na kupata mateso makubwa kutokana na hilo, na aiwezeshe Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida. Khilafah ambayo ndani yake Takbira za Idd zitachanganyika na Takbira za kuitakasa Gaza na Palestina yote kutokana na uchafu wa ndugu wa manyani na nguruwe, na Kashmir kutokana na uchafu wa Mabaniani, na ardhi zote za Kiislamu zilizokaliwa kwa mabavu, na kuziregesha kwenye kumbatio la Umma wa Kiislamu, kwa Takbira za kunyanyua juu zaidi bendera ya Al-‘Uqab katika ardhi zote, mikono mwa Khalifa muongofu Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, akitangaza kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Vile vile tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu afungue nyoyo na akili katika Mashariki na Magharibi ili kuukumbatia Uislamu, kuwatoa katika ibada ya viumbe na kuwapeleka katika kumwabudu Mola wa viumbe, baada ya ulimwengu kugeuzwa jahannam na mfumo wa kibepari, ukitenganisha Dini na maisha, kudhalilisha wanadamu hadi viwango vya kinyama, na kujifakhirisha juu ya kukuuza machafu na upotofu, na kuyalingania pasi na aibu mbele ya Mwenyezi Mungu au waja wake; ili dunia ijae uadilifu baada ya kuungua kwa muda mrefu chini ya moto wa mfumo gandamizi na dhalimu wa kibepari, ambao sasa unashuhudia mporomoko mkubwa usio na kifani wa kiuchumi unaoikabili dunia kutokana na kuondolewa kwa kiwango cha dhahabu katika miamala ya kifedha na kuifunga kwa fedha za karatasi zisizo na thamani ya dhati, na kusababisha hasra kwa mali za watu.

Tangu kuanguka kwa taji la faradhi zote, Dola ya Khilafah, sherehe za Idd zimechanganyikana na maumivu na uchungu kutokana na mateso ya Ummah. Matukio tunayoyaona leo katika Gaza Hashim yanapaswa kuwachochea wasongaji katika Ummah, majeshi yake, wanazuoni, vyama vya kisiasa, vijana, na watu wa vyombo vya habari kuelekea kwenye lengo tukufu, ambalo ni kuling'oa umbile la Kiyahudi na wale watawala wanaosimama kama kizingiti.

Kwa kumalizia, tunapenda kuteka hisia za watu mashuhuri wa vyombo vya habari na watu wenye ushawishi ili kuangazia suluhisho ambalo linaokoa wanadamu wote, ambalo liko mbele yenu na ndani ya ufikiaji wenu: ni kuutekeleza Uislamu katika maisha halisi. Hizb ut Tahrir iko miongoni mwenu, mizizi yake ni ya kina, na matawi yake ni ya juu sana. Msiiwache Magharibi na watawala washirika wake wakupurukusheni kutokana nalo au kutokana na kuangazia kadhia nyeti za Waislamu. Tazameni matukio kupitia jicho la itikadi la Kiislamu.

Mwenyezi Mungu azikubali ibada za mahujaji kwenye Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu na amali njema za wale wasiofanya hija. Idd Mubarak kwenu nyote, na mujikurubishe kwa Mwenyezi Mungu. Ewe Mwenyezi Mungu, iharakishe afueni na utufurahishe kwa ushindi mkubwa:

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu…” [Surat Ar-Rum:4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb utTahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizbuttahrir.today
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu