Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 503
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kalima kutoka kwa Ustadh Mahmut Kar, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki, akiwawajibisha wahalifu waliowasha moto wa ufisadi katika mji wa Uturuki wa Kayseri baina ya wahamiaji wa Syria na wakaazi wa Uturuki ambao umeenea hadi miji mingi ya Uturuki.
Jana, Jumamosi, tarehe 6 Julai 2024, lile linaloitwa Kongamano la Kisiasa na Majeshi ya Kiraia ya Sudan lilifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo; nukta muhimu katika taarifa ya mwisho zilizotolewa zilikuwa: “...wanakongamano pia walisisitiza ulazima wa kushikamana na Azimio la Jeddah na kuzingatia taratibu za utekelezaji na maendeleo yake ili kuendana na maendeleo katika vita…
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 2024 kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov. Mashababu hao tayari walikuwa washatumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 mwaka huu kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov, ambayo kwayo walitumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.
Bajeti ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa imezua Balaa kwa Waislamu! Hukmu za Uislamu ndizo pekee zilizo na uwezo wa kuhafifisha migogoro mikubwa ya kiuchumi.
Khilafah itakomesha sera ya ubinafsishaji iliyowekwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, IMF, ambayo imesababisha uharibifu wa sekta ya nishati, mafuta na gesi, na badala yake itatabikisha hukmu ya umilikaji wa umma katika Uislamu, kuhusiana na nishati na madini.
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni taasisi ya kikoloni ikitoka kwa mkataba wa bretton woods, inatumika kuanzisha ukiritimba wa dola ya marekani katika biashara ya kimataifa.
Kwa kutenga asilimia 52 ya bajeti yote kwa malipo ya riba pekee, maslahi ya wananchi, serikali na usalama yako hatarini.