Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 536
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Shirika la habari la Reuters liliripoti mnamo Februari 21, 2025 kwamba “Marekani imetoa dolari milioni 397 kusaidia mpango wa kijeshi katika chini ya Pakistan yenye silaha za nyuklia, huku msaidizi mmoja wa bunge akisisitiza kwamba matumizi ya F-16 ya Marekani katika operesheni za kukabiliana na ugaidi yatafuatiliwa isipokuwa dhidi ya India.” Huu ndio uhalisia wa ukoloni wa kijeshi: kuyafanya majeshi ya Waislamu kupigana wao kwa wao, huku wakiyazuia kupigana jihad dhidi ya India, umbile la Kizayuni, na majeshi ya Msalaba!
Dola ya Kiislamu imeegemezwa kwenye Aqidah (itikadi) ya Kiislamu, na hili linahitaji kwamba katiba yake na sheria zake zote zichukuliwe kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw).
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina), na kwa kuzingatia matakwa ya adui wa Mwenyezi Mungu, Trump, kuwahamisha Waislamu wasio na ulinzi kutoka Ukanda wa Gaza, Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki inaandaa amali za halaiki kote nchini Uturuki chini ya kichwa: “Ni Nani atamzuia Trump?!”
“Mapema leo, Rais Trump wa Marekani alithibitisha mpango wake wa Marekani kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwafukuza Wapalestina, akisema kwamba amejitolea kuinunua na kuimiliki Gaza. Kauli hii ilitolewa na Trump mnamo Jumapili jioni ndani ya ndege ya Air Force One alipokuwa akielekea New Orleans kuhudhuria Super Bowl." (BBC, 10/2/2025) Baadaye, wakati wa mkutano wake na Mfalme wa Jordan, alisema: "Wapalestina wataishi kwa usalama mahali pengine, nje ya Gaza, na ninaelewa kwamba tuna uwezo wa kufikia suluhisho,"
Trump na Mfuasi wako Netanyahu: Macho Yako Yamepofushwa, umesahau hatima ya watangulizi wako miongoni mwa Warumi na Wafursi, pamoja na washirika wako duni, Mayahudi!
Ripoti ya jibu la swali lililotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kuhusu Kuongezeka kwa Uhasama nchini Sudan.
Ramadhan ni mwezi ambao ndani yake Umma wa Kiislamu ulishinda maadui wengi wenye nguvu. Hebu Waislamu na waregeshe hukmu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ﷻ katika mwezi wa Ramadhan, na warudishe ushindi dhidi ya maadui, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ.