Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 China na Amerika: Katika Mahusiano Changamani

(Imetafsiriwa)

Hivi karibuni Bunge la Amerika limeidhinisha bajeti ya ulinzi ya dolari bilioni 777.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia tano kutoka mwaka jana. Hatua hii imekuja baada ya kuondoshwa vikosi vya mwisho vya Amerika kutoka Afghanistan na imehalalishwa kuwa ndio njia ya kushughulikia ushindani unaoongezeka na China. (Al Jazeera)  Kuidhinishwa kwa bajeti kumeungwa mkono na vyama vyote viwili na kuunga mkono msimamo wa sasa wa Amerika kuwa China inatoa kitisho kikubwa kwa ubwana wake wa dunia.

“Serikali ya China inataka kuwa dola kubwa zaidi kupitia ukopeshaji wa kinyang'anyi na njama za kibiashara, wizi wa kimfumo wa milki za ubunifu wa akili, na udukuzi kwenye mfumo wa kompyuta” (Chanzo: FBI website)

Lakini uchambuzi wa historia na muundo wa mfumo wa kimataifa, pamoja na dori ambayo Amerika na China wanacheza ndani yake, inaonyesha kuwa hali haiko nyepesi kama Amerika inavyoonyesha.

Tunapotathmini mahusiano baina ya mataifa, hatuwezi kupuuza namna ambayo mfumo wa kimataifa umewekwa kuanzia katikati hadi mwishoni mwa karne ya 20. Amerika imeibuka kuwa ndio dola kiongozi na imeweka mfumo wa kimataifa katika taasisi za kimataifa, muingiliano wa kiuchumi na maadili na kanuni za kiliberali. Yote haya yamekubaliwa na mataifa yenye nguvu wakati huo na kile kilichoibuka ilikuwa ni hali ambayo wote wamekubali kusuluhisha matatizo yao na kutatua masuala ya maslahi ya kitaifa, bila ya kuingia kwenye vita kama ilivyokuwa wakati wa zama za kibeberu. Mfumo wa sasa wa kimataifa umefungwa na Amerika – na hivyo kila nchi ina hamu katika kuhakikisha kuwa Amerika inabaki tulivu na kudhibiti ushawishi wake.

Wakati Ukomunisti ulipoanguka na China kuchagua kuingia katika mfumo wa kimataifa, imekubali kuyafanyia kazi maadili na kanuni ambazo Amerika imeziweka na kuufanya Urasilimali kuwa ndio mfumo wake. Wakati ikizidi kuunga mkono fikra za kiimla ndani ya mipaka yake, matendo yake katika medani za kimataifa yanaendelea kuonyesha kuwajibika kwake na mfumo wa kiulimwengu wa kirasilimali.

Kwa kufanyakazi kwake ndani ya mfumo wa kimataifa, bila kukusudia wameunga mkono Amerika na dori yake kama ni dola kiongozi.

Uchina imeendelea kukazania ‘kukua kwake kwa amani’ kwani imeendelea ndani ya miaka michache iliyopita na imekuwa muangalifu kujionyesha kuwa ni watetezi wa utandawazi na biashara huru. Tokea kwenye miaka ya 1980 wamejifungamanisha na kuendana kwa kiasi kikubwa na taasisi kubwa na kanuni za mfumo wa kimataifa. Na raisi Xi amekuwa akirejelea miito ya kujenga uchumi wa kiulimwengu wa uwazi zaidi na kupingana na vikwazo vya kibiashara mara kadhaa tokea muda huo (Global Times, 2019). Wakati kukiwa na mivutano, nchi hizo mbili zimekuwa na utegemeano mkubwa wa kiuchumi ambao hauwezi kubezwa. Utegemeano huu maana yake ni kuwa nchi zote zitakabiliana na madhara pindi nchi moja wapo ikijaribu kuidhuru nyengine, na China inatambua hilo.

“Mnamo mwaka 2009 Jeshi la Watu wa China liliitaka serikali ya China kuuza baadhi ya akiba ya dolari zake kuiadhibu Amerika kwa kuiuzia silaha Taiwan. Benki ya Watu wa China ikatanabahisha kuwa kwa kufanya hivyo itapelekea hasara kubwa kwa China. Serikali ikawa pamoja na ushauri wa benki kuu. Kuanguka kwa ghafla kwa dolari kunaweza kuifanya Amerika kupiga magoti, lakini pia itakuwa na matokeo ya uharibifu kwa China. Vile vile, katika mazingira ya sasa ambayo yanagubika uvamizi wa kimtandao wa China kwenye gridi ya nguvu za umeme wa Amerika, utegemeano wa kiuchumi wa nchi mbili utamaanisha madhara ya hasara kwa China vile vile. Vamizi zenye kulenga maeneo maalum madogo madogo ya kiuchumi huenda hazitozaa hasara ya moja kwa moja, lakini kuongezeka kwa umuhimu wa intaneti katika ukuaji wa uchumi kunaongeza vivutio jumla kwa uwezo wa kujisimamia mambo yake. Uhalali wa chama cha Kikomunisti cha China kinategemea zaidi ukuaji wa kiuchumi, na ukuaji wa uchumi nchini China unaendelea kutegemea zaidi intaneti.” (Financial Times)

Uchina imejiweka kuwa ni kitovu cha uzalishaji na uchumi unaotegemea usafirishaji nje wa bidhaa. Hii ina maana kuwa imetegewa ndani ya mfumo wa kiuchumi wa kimataifa, na kwa kuwa mfumo wa kiuchumi umefungwa na dolari, China inaitegemea Amerika kwa kiasi kikubwa. Wanasafirisha bidhaa nyingi zaidi na huduma Amerika kuliko Amerika inavyouza kwa China. Wameliweka deni la Amerika katika kiwango cha kimataifa kuhakikisha ushindani wa bei kwa mauzo yake ya nje- Mnamo Jan 2021, China iliidai US dolari trilioni 1.095, au ni kiasi asilimia 3.7 ya deni la taifa la US la dolari trilioni 29, ambalo ni zaidi ya deni la nchi nyengine ya kigeni isipokuwa Japan.

Hatimaye, nchi zote mbili zinategemeana. Mnamo 2020, China ilikuwa ni mshirika mkubwa zaidi wa bidhaa za biashara, nchi ya tatu kwa kuwa na soko kubwa la mauzo ya nje, na chanzo kikubwa zaidi cha manunuzi kutoka nje. Mauzo ya nje kuelekea China yametoa nafasi za kazi kiasi ya watu milioni 1.2 nchini Amerika mwaka 2019. Makampuni mengi zaidi ya Amerika yaliopo China yamewekeza kwenye soko la China kwa kipindi kirefu kijacho. (Brookings)

Wakati China inaelekea kuchukua hatua za kuusokotoa uchumi wake na kupunguza utegemezi wake kwa Magharibi, suala la kuwa mfumo mzima wa uchumi umefungwa kwenye dolari, inamaanisha kuwa Amerika muda wote itadhibiti nafasi muhimu ndani ya mfumo wa sasa wa kimataifa. Hivyo China itabidi kufuata hatua kwa uangalifu kutokana na mahusiano baina ya maendeleo yake ya ndani na uchumi wa kimataifa. Kwa sababu ili iweze kufanya mabadiliko, China itahitaji kuzishawishi nchi nyengine za dunia kuikubali dhidi ya Amerika – jambo ambalo bado haijalifanya.

Hii haina maana kuwa hakutakuwepo na mivutano baina ya mataifa haya mawili. Katika mfumo wa Kirasilimali, muda wote kutakuwepo na mivutano kutokana na maslahi yao ya kitaifa na mchezo mgumu wa kisiasa, lakini mataifa haya yameonyesha kuwajibika kufanya kazi ya kuiondoa mivutano hiyo kwa namna ambayo haiathiri mfumo wa kimataifa- Uchina ni mwanachama wa taasisi kadhaa za kimataifa kama Shirika la Biashara la Dunia (WTO) na muhimu zaidi, ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mambo yanabadilika ndani ya mfumo wa kimataifa, hivi sasa mataifa yanahitaji kuangalia kama yanaweza kujifungamanisha na kushughulika nao. Lakini Amerika bado itabaki kudhibiti nafasi yake na kufanya kazi ya kuibakisha.

Dunia imepitia mabadiliko mengi na imekumbana na changamoto nyingi. Inahitaji kujifungamanisha nao lakini hiyo haimaanishi kuwa Amerika itaachia nafasi yake ya kuwa dola kuu- ina maana tu ya kuwa mataifa mengine yanaendelea ndani ya mfumo ambao imeuweka na kudhibiti na kuhifadhi maslahi yao ya kitaifa ndani ya mfumo huo. Wakati Amerika ilipochagua kuongeza bajeti yake ya kijeshi, imezihakikishia nchi za kirasilimali kuwa bado inabakisha kwa umakini dori yake ya kuwa ni dola kiongozi na iko tayari kufanya maamuzi yatayoiruhusu kuulinda mfumo wa kimataifa, ili kwamba wote waendelee kuunga mkono.

Ni lazima pia tukumbuke kuwa yeyote anayeibuka kuikabili Amerika ni lazima akubali kuingia kwenye mivutano na mataifa mengine- ambayo yapo tayari kuulinda mfumo wa Kirasilimali, ambao Amerika imejifunga nao. Hii itazifanya nchi nyengine kusitasita kufuata malengo ya dunia na kuwa na hadhari wakati zikifuata malengo ya kimaeneo.

Mvutano unaofuata wa kimataifa utakuwa ni baina ya mifumo – Uislamu na Urasilimali, na sio China na Amerika

Kwa kujikubalisha na mfumo aina moja, mataifa yanakwenda sambamba na maslahi yao. Uovu wa mfumo wa Kirasilimali unaendelea kuwa wazi, na matokeo yake mataifa yanaendelea kukata tamaa kubakisha mamlaka yao.

Mvutano wa mwisho wa kimataifa ulikuwa baina ya Urasilimali na Ukomunisti. China sio tena nchi ya Kikomunisti – inaweza kuunga mkono baadhi ya maadili yake lakini haijafuata mfumo wake kama USSR ilivyofuata mwanzoni. Hivi leo, kitovu cha sera zake (hata zile za CPEC) ni kuhakikisha kuwa inadhibiti maendeleo yake ya kiuchumi na inamudu kupunguza uingiliaji wa Amerika katika maeneo ya maslahi ya kitaifa na kieneo. Lakini mwishowe, ni nchi ya Kirasilimali ingawa sio ya kiliberali.

Mvutano ujao utakuwa baina ya Uislamu na Urasilimali, kama ambavyo mataifa yatafahamu kuwa kusimamishwa tena kwa Dola ya Kiislamu kutamaanisha mwisho wa udhibiti wa kimataifa, kama Maquraysh walivyofanya wakati wa Mtume (saw).

Thauban ameripoti kuwa Mtume (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِي الْأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الْأَحْمَرَ وَالْأَبْيَضَ وَإِنِّي سَأَلْتُ رَبِّي لِأُمَّتِي أَنْ لَا يُهْلِكَهَا بِسَنَةٍ عَامَّةٍ وَأَنْ لَا يُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُوًّا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ وَإِنَّ رَبِّي قَالَ يَا مُحَمَّدُ إِنِّي إِذَا قَضَيْتُ قَضَاءً فَإِنَّهُ لَا يُرَدُّ وَإِنِّي أَعْطَيْتُكَ لِأُمَّتِكَ أَنْ لَا أُهْلِكَهُمْ بِسَنَةٍ عَامَّةٍ وَأَنْ لَا أُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُوًّا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ يَسْتَبِيحُ بَيْضَتَهُمْ وَلَوْ اجْتَمَعَ عَلَيْهِمْ مَنْ بِأَقْطَارِهَا أَوْ قَالَ مَنْ بَيْنَ أَقْطَارِهَا حَتَّى يَكُونَ بَعْضُهُمْ يُهْلِكُ بَعْضًا وَيَسْبِي بَعْضُهُمْ بَعْضًا»

“Mwenyezi Mungu amenisogezea pembe za dunia nikaona mashariki yake na magharibi yake. Na hakika utawala wa Ummah wangu utafikia pembe zote nilizosogezewa na nimepewa hazina mbili nyekundu na nyeupe na nimemuomba Mola wangu kwa ajili ya Ummah wangu kuwa usiangamizwe kwa sababu ya ukame, wala usisalitiwa na adui ila aliye miongoni mwa Ummah na kuangamiza maisha yao na kuwateketeza kabisa, na Mola wangu amesema: Ewe Muhammad, Mimi nimefanya maamuzi basi hayarejeshwi, Nimekupatia wewe kwa ajili ya ummah wako kuwa hautohilikishwa kwa ukame na hautosalitiwa na adui ila aliye miongoni mwa Ummah na kuangamiza maisha yao na kuwateketeza kabisa, hata kama watu wote kutoka sehemu tafauti za dunia wataungana” [Muslim].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu