- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Gaza Inahitaji Majeshi Kuwapindua Watawala na Kutangaza Jihad”
Matembezi yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 13 Shawwal al-Khair 1446 H sawia na tarehe 11 Aprili 2025 M kuanzia Msikiti wa Al-Fath kunusuru watu wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa ulio mateka, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunisia chini ya kichwa: “Gaza Inahitaji Majeshi Kuwapindua Watawala na Kutangaza Jihad” na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu wa Tunisia ya kijani, ambayo yalizunguka barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likiwa na kichwa cha matembezi, na bango jengine likiandikwa “Mashahidi 51,600, watoto 18,000 na wanawake 12,000. Basi mtafanya nini enyi majeshi ya Waislamu?” Makumi ya mabango mengine pia yaliinuliwa, yakitoa wito kwa majeshi ya Waislamu katika nchi za Kiislamu kuwanusuru ndugu zao nchini Palestina. Maandamano hayo yalijumuisha kauli mbiu zilizokuwa zikiimbwa na umati mkubwa wa watu, kama vile “Umma unataka kutangazwa Jihad,” “Umma unataka kuangusha viti vya utawala,” “Umma unataka kuvunja mipaka,” na kauli mbiu nyenginezo, nyingi zikiwahutubia maafisa na wanajeshi katika majeshi ya Waislamu, zikiwakumbusha wajibu wao kwa ndugu zao wanaokandamizwa mjini Gaza. Matembezi hayo yalihitimishwa kwa hotuba iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir, ambapo aliyakumbusha majeshi ya Waislamu juu ya udharura wa kuwanusuru ndugu zao wa Palestina baada ya kuviangusha viti vya watawala madhalimu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 13 Shawwal Al-Khair 1446 H sawia na 11 Aprili 2025 M
- Video ya Sehemu ya Amali ya Matembezi -
- Picha za Amali ya Matembezi -
https://hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/tunisia/4631.html#sigProIde14a95bff4
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir