Mabinti wa Ummah Wanauawa mbele ya Macho Huku Ulimwengu Unasikiliza
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wakati makumi ya maelfu ya raia wa Gaza wakikimbilia kusini, kutafuta usalama kwenye mpaka wa Rafah na Misri, hadithi moja ya jaribio la kutoroka inadhihirika: ile ya Hind Rajab mwenye umri wa miaka 6. Alikuwa njiani na wanafamilia wengine kukutana na mama yake wakati gari la Kia walilokuwa wakisafiria liliposhambuliwa na Majeshi ya umbile la Kiyahudi, na familia zote zilizokuwa kwenye gari hilo ziliuawa.