- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Si Mageuzi ya Uchaguzi wala ya Katiba Yatakayoikomboa Tanzania
(Imetafsiriwa)
Habari:
Wakati Tanzania ikitarajia kuwa na Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, wimbi la mgawanyiko wa kisiasa na mitazamo tofauti kuelekea uchaguzi huo lipo miongoni mwa wanasiasa na vyama vya kisiasa ambalo limezua mjadala mkubwa wa kisiasa.
Maoni:
Mazingira ya sasa ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu baadaye mwaka huu nchini Tanzania yameleta mitazamo mitatu mikuu ya kisiasa ambayo imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na makundi mbalimbali ya watu kote nchini.
Kundi la kwanza ni wale wanaosisitiza haja ya haraka ya mageuzi ya uchaguzi yaliyoanzishwa na chama kikuu cha upinzani-Chadema chini ya kauli mbiu yao, "Hakuna Marekebisho Hakuna Uchaguzi." Msimamo huu una mtazamo kwamba bila kuwepo kwa mageuzi, uchaguzi hautakuwa huru na wa haki na unapaswa kususiwa. Wengine ni wale wanaoomba marekebisho ya katiba yanayopigiwa debe na chama cha pili cha upinzani - ACT Wazalendo. Msimamo huu unasisitiza marekebisho ya katiba, lakini tofauti na Chadema, chama hiki hakiko katika nafasi ya kususia uchaguzi.
Kundi la tatu ni wale wanaounga mkono hali halisi iliyopo (serikali). Hawaoni umuhimu wa usimamizi wa uchaguzi na katiba. Wanaunga mkono katiba ya sasa, kanuni na taratibu za uchaguzi. Kundi hili liko chini ya ushawishi wa serikali iliyopo madarakani na chama tawala - CCM.
Makundi yote matatu ya wanasiasa, vyama vya kisiasa na wafuasi wao wanapaswa kujua kwamba kamwe hawatapata manufaa yoyote kwa nchi, watu kama wanavyodai wote.
Ama kuhusu wale wanaounga mkono mageuzi ya uchaguzi, wanapaswa kukumbuka kwamba kumekuwa na mageuzi mengi ya uchaguzi hapo awali, kama vile ya 2010, 2019 na mageuzi ya hivi majuzi zaidi ya 2023 - Sheria ya Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi 2023. Hakuna hata moja iliyofanya kazi.
Kwa wale wanaounga mkono mageuzi ya katiba wakioongozwa na chama cha pili cha upinzani cha ACT-Wazalendo, kampeni ambayo ilizinduliwa pia mwaka 2024, tunapenda kuwakumbusha pia kwamba, Tanzania tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1961 imepitia mageuzi na marekebisho mengi ya katiba ya mwaka 1961, 1962, 1964, 1965, na 1977. Zanzibar kwa upande mwengine pia ilikuwa na mageuzi mnamo 1963, 1979 na 1984. Tangu wakati huo kumekuwa na mfululizo wa marekebisho mengi katika sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hakuna iliyofanikiwa.
Kwa wale wanaounga mkono hali halisi iliyopo, wafuasi wa chama tawala CCM na serikali iliyopo madarakani walioridhika na kanuni za sasa za uchaguzi na katiba za sasa, hawako kwenye upande salama pia, kwani udhaifu wa kanuni na katiba za sasa unaonekana wazi kwa kila mtu.
Makundi yote matatu yameshindwa kuelewa chanzo kikuu cha tatizo ambacho si kanuni za uchaguzi, katiba au upinzani (kwa wanaounga mkono serikali). Chanzo kikuu ni mfumo wa ubepari ambapo kanuni na sheria zote za sasa nchini Tanzania na mataifa yanayoendelea ni za kigeni na za kikoloni. Kupitia kanuni na sheria hizi za kibepari, ukoloni mamboleo unalazimishwa nchini Tanzania na nchi zinazoendelea; kuwezesha mataifa ya kibepari kuyanyonya mataifa haya.
Hivyo basi, mabadiliko yenye natija ya kuikomboa Tanzania na kwengineko yanapaswa kuelekezwa katika kuondoa mfumo mchafu wa ubepari kwa kuubadilisha na Uislamu chini ya uongozi wake wa kilimwengu (Khilafah).
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania