- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jinsi Viongozi wa Waislamu Wanavyoitelekeza Gaza kwa ajili ya Diplomasia na Miamala
(Imetafsiriwa)
Habari:
Rais wa Indonesia Prabowo Subianto alihimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja kati ya 'Israel' na Hamas, na akatoa wito wa kusitishwa kwa mzozo wa 'Israel' na Iran. Akizungumza nchini Singapore na Waziri Mkuu Lawrence Wong, Prabowo alisisitiza haja ya azimio la amani kupitia diplomasia. Alionyesha wasiwasi wake mkubwa juu ya vifo vya raia huko Gaza na kuongezeka kwa mvutano katika Mashariki ya Kati. Zaidi ya hayo, alizungumzia mzozo wa Myanmar, akisisitiza kujitolea kwa ASEAN kwa Makubaliano ya Mambo Tano ya kukomesha vurugu na kukuza mazungumzo jumuishi. Indonesia na Singapore zilikubali kuendelea kuunga mkono ushirikiano wa amani nchini Myanmar na kuzingatia kanuni za ASEAN za uthabiti wa kikanda na juhudi za kibinadamu. (Antara news)
Maoni:
Tangu kuzuka kwa vita vya 2023, serikali ya Indonesia imeichukulia kadhia ya Palestina kama hotuba ya kisiasa tu, isiyo na hatua halisi na thabiti. Kwa hakika, mahusiano ya kibiashara kati ya Indonesia na umbile la Kizayuni yameendelea bila kukatizwa.
Hili linaakisi majibu ya viongozi kadhaa wa Waislamu wa Waarabu, ambao wanaonekana kujifanya wanajali kadhia ya Palestina na kulaani hadharani vitendo vya Wazayuni, lakini wanashindwa kuchukua hatua zozote za kimsingi kukomesha mauaji ya Waislamu wenzao huko Palestina.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba, viongozi hawa wameonyesha uwiano unaoongezeka na Marekani—kukaribisha mapokezi ya dhati na kuahidi uwekezaji mkubwa, hasa katika ziara ya Trump Mei 2025. Hili linatia wasiwasi sana, kwani Marekani ndiyo mwezeshaji mkuu wa utawala wa Kizayuni, daima ikitoa silaha zinazotumiwa katika mauaji ya raia wa Gaza.
Wakati Iran iliposhambuliwa na umbile la Kizayuni, nchi jirani za Waislamu nazo zilibaki kimya. Katika baadhi ya matukio, walishirikiana na wanajeshi wa Kizayuni na Marekani kuzuia makombora ya Iran. Kimsingi, kulipiza kisasi kwa Iran kulipaswa kuhimiza mshikamano mpana wa Kiislamu ili kudhoofisha muungano wa Kizayuni na Marekani. Kwa bahati mbaya, fursa hii ilipuuzwa kutokana na upofu wa serikali hizi kuuona ukweli.
Hadi sura ya kisiasa ya kisekula ya ulimwengu wa Kiislamu ibadilike, kuna matumaini machache ya hatua za kweli katika kuwatetea watu wa Palestina au kuwalinda Waislamu kote duniani.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar