Alhamisi, 01 Muharram 1447 | 2025/06/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wadhifa wa Rais eneo la Asia ya Kati ni Sawia na Ufalme

(Imetafsiriwa)

Habari:

Shirika la habari la Radio Liberty liliripoti mnamo tarehe 29 Mei: "Putin alifanya mazungumzo na Rustam Emomali, mwenyekiti wa bunge kuu la Tajikistan. Katika mfumo wa ziara yake rasmi jijini Moscow, Mwenyekiti wa Majlisi Milli Majlisi Oli ya Tajikistan na Meya wa Dushanbe Rustam Emomali walifanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin, Spika wa Baraza la Federali Valentina Matvienko na Mwenyekiti wa Jimbo la Duma Vyacheslav Volodin.

Mazungumzo hayo yaliangazia katika kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, kuendeleza mazungumzo baina ya mabunge, kupanua ushirikiano wa kibinadamu na masuala ya uhamiaji wa wafanyikazi, ukurasa wa Facebook wa Majlisi Milli uliripoti.”

Maoni:

Hii sio ziara ya kwanza ya mtoto wa dikteta E. Rakhmon nchini Urusi. Mkutano huu ulikuwa na sherehe rasmi zaidi na ulikuwa mandhari ya ukumbusho zaidi. Dhalimu E. Rakhmon tayari ana miaka mingi na afya yake inadhoofika, jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa kwa haraka kwa mgombea wa rais mpya wa nchi. Asia ya Kati imekuwa na imesalia chini ya udhibiti wa Kremlin kwa zaidi ya miaka 100, kwa hivyo madikteta wa jamhuri hizi hutuma warithi wao kwa Kremlin ili kupata idhini au uhakiki wa kugombea wadhifa wa rais wa nchi.

Tunaweza kuona mandhari kama hiyo ya uhamishaji wa mamlaka kutoka kwa mtawala wa Turkmenistan Gurbanguly Berdymukhamedov hadi kwa mtoto wake Serdar Berdymukhamedov.

Berdymukhamedov alirithi mamlaka kutoka kwa babake mwaka wa 2022. Miaka michache kabla ya hapo, Serdar alipitia hatua kadhaa za mageuzi ya kuwa mamlakani, kama vile meya wa eneo hilo, nyadhifa za mawaziri, wadhifa katika baraza la usalama, nk. Kwa muda fulani, babake Serdar alisafiri naye kwenye mikutano rasmi, kama uzio dhidi ya kupoteza mamlaka, lakini akiwa na hakika kwamba kila kitu kilikuwa kikienda kwa uhuru kulingana na maandishi yake, Gurbanguly alimuacha mtoto wake aende ‘kuogelea kwa uhuru’. Kwa hivyo, mamlaka yalipitishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mwana.

Tofauti na marais wa Turkmenistan na Tajikistan, marais wa Uzbekistan na Kazakhstan, wa zamani na wa sasa, wana wasichana kama warithi, ambayo inafanya kuwa vigumu uhamishaji wa madaraka. Haikubaliki katika utamaduni wa Asia ya Kati kwa mwanamke kuwa raia wa nchi. Lakini pamoja na hayo, kama tulivyoona, mabinti wa madhalimu wamekuwa wakifanya kazi katika maisha ya kisiasa ya serikali. Sio zamani sana, binti za Karimov na Nazarbayev walishiriki katika karibu michakato yote ya kiuchumi ya nchi. Leo, binti ya Mirziyoyev sio tu anashiriki katika siasa za ndani za nchi, lakini hata anawakilisha Uzbekistan nje ya nchi.

Katika historia ya kisasa ya Asia ya Kati, mila mpya imeanzishwa kwamba mtu yeyote anayekuwa rais wa nchi anachukua matawi yote ya mamlaka, akiweka jamaa zake katika nafasi zenye ushawishi na kurithisha mamlaka, kama inavyotokea katika ufalme. Wakiwa juu, watawala wenye uchu wa madaraka hawashiriki nao, isipokuwa katika hali ya kifo au dharura. Wakiwa madarakani, familia nzima inatesa watu kwa ukandamizaji na dhulma.

Sisi ni Waislamu wa Asia ya Kati, na sisi ni wageni kwa mifumo ya serikali isiyo ya Kiislamu kama vile jamhuri au falme. Katika Uislamu, mamlaka ni ya Ummah, na utawala na maamuzi ni ya Shariah, si ya watu na si ya Khalifa. Ummah humchagua Khalifa kutabikisha Shariah ardhini na kutawala kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake kitukufu:

[إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ] “Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu.” [6:57],

[وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللّهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ] “Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [5:50],

[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللّهُ إِلَيْكَ * فَإِن تَوَلَّوْاْ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.” [5:49]

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliasisi Dola ya Kiislamu mjini Madina Al-Munawwara na akatuonyesha njia bora ya kuunda vyombo vya dola. Aliwateua Magavana wa wilaya, makadhi wa miji, akachagua wasaidizi wake na akaunda Majlis al-Shura. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akawa kiongozi wa dola hii kama mtawala, na Maswahaba zake (ra) wakamwapia kiapo cha kuwa kama mtawala. Baada ya kifo cha Mtume (saw) kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, maswahaba watukufu waliendelea na kazi hii. Watawala waliitwa Khulafaa’ (Makhalifa) na mfumo wa utawala uliitwa Khilafah.

Kukombolewa kwetu kutokana na watawala madhalimu wasiotawala kwa mujibu wa sheria za Uislamu ni katika kufanya kazi kwa mujibu wa njia ya Utume, ili kuhuisha Dola ya Pili ya Khilafah Rashida inayoongozwa na mtawala muongofu Khalifa. Khalifa ambaye atatawala kwa mujibu wa sheria za Mwenyezi Mungu, akiangamiza udhalimu na uovu, akieneza nuru ya uadilifu wa Uislamu duniani. Twamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Ziara ya Usaliti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu