Ijumaa, 03 Muharram 1447 | 2025/06/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Erdoğan anapaswa Kuhutubia Umma wenye Ikhlasi na sio Walinzi wa Sykes-Picot kwa Umoja na Udugu wa Kiislamu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akihutubia Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu jijini Istanbul, Rais Recep Tayyip Erdoğan ametoa wito wa kuwepo umoja na udugu mkubwa zaidi miongoni mwa nchi za Kiislamu. Erdoğan pia alisema, "Hatutaruhusu kuanzishwa kwa agizo jipya la Sykes-Picot katika eneo letu mipaka kuchorwa kwa damu." Na alisisitiza kwa mara nyengine kwamba suluhisho liko katika "diplomasia na mazungumzo".

Maoni:

Je, ni aina gani ya umoja na udugu ambao Erdoğan anautaka? Na ana matumaini gani ya kuanzisha umoja huu?

Msisitizo wa Erdoğan juu ya "suluhisho kupitia diplomasia na mazungumzo" kwa mara nyengine tena ni usemi wa hamu yake tu ya kuhifadhi "utaratibu uliopo wa Sykes-Picot".

Vikwazo vilivyo mbele ya umoja na udugu katika Uislamu kwa hakika ni mipaka ya "Sykes-Picot" ambayo tayari imechorwa kwa damu, na dola za kitaifa zilizowekwa ndani ya mipaka hii, na tawala bandia za Magharibi, ambazo zinalinda dola hizi za kitaifa. Umoja na udugu wa Kiislamu hauwezi kujengwa kupitia mazungumzo kuhusu utaifa, mipaka ya nchi, au ulinzi wa mipaka ya Uturuki, Iran, Palestina, Syria nk, na si kwa kukandamiza umoja wa Waislamu katika Iman chini ya kitambulisho cha kitaifa. Palestina, na hasa Gaza, ni ushahidi wa wazi wa hili. Kwa kuwa mipaka yake imechorwa na Sykes-Picot, kwa pingu za Lausanne, katiba yake ya kubandikwa kutoka nchi za Magharibi, sera zake za ndani na nje zilizoamriwa na mikataba ya kimataifa, na kwa kuwa nchi ya kwanza ya Kiislamu kumtambua katili wa Kizayuni kama dola ya halali kwa ajili ya kuwaridhisha mabwana zake wa Kimagharibi, je, Jamhuri ya Uturuki haitumiki kama ushahidi wa wazi zaidi wa khiyana ya udugu huo?

Je, Erdoğan alichangia nini katika udugu wa Kiislamu tangu alipokuwa waziri mkuu wa Uturuki mwaka wa 2003 na kisha rais mwaka wa 2014? Tuweke usaliti wake nchini Misri na Syria kando kwa sasa. Tangu "Dakika Moja" yake maarufu! na "Al-Quds ni msitari wetu mwekundu", aliwasaliti mashahidi wa Mavi Marmara Flotilla, huku akizidisha kiwango cha biashara ya Uturuki na Wazayuni mara kumi na moja. Huku akitamka maneno mengi ya kuhuzunisha moyo kuhusu Gaza, alikidhi mahitaji yote ya "Nazi", kama anavyomtaja gaidi huyo, alilishwa kwa petroli, chuma, buti za kivita, vifaa na vyakula vya wazungu, huku akipitisha matatizo ya Waislamu kwa waundaji wa "Sykes-Picot", ambao huvunjavunja Umma vipande vipande. Kwa hakika, Erdoğan, ambaye anafanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hii ya Sykes-Picot - haswa "kampuni ya huduma kwa Mzayuni" - hakufanya chochote kwa wahudumu wa afya wa Gaza, ambao walichomwa moto wakiwa hai, madaktari wake, ambao wanateswa katika jela la Wazayuni, mama zake, ambao walifanyiwa upasuaji wa kuzaa bila dawa za ganzi, na watoto wake ambao walikatwa miguu bila dawa za ganzi, watoto wake wenye njaa, wanaochomwa moto wakiwa hai.

Hii, licha ya kuwa na jeshi la 9 lenye nguvu zaidi duniani na la 4 la NATO lililosimama imara zaidi, licha ya kuwa na mkwe, ambaye huzalisha UAV na UCAV za juu zaidi duniani, na ndege za kivita za kisasa; badala yake, anapayukwa itikadi za wahubiri wa "Sykes-Picot" - anasisitiza kwamba suluhisho "liko ndani ya diplomasia na mazungumzo" na "suluhisho la dola mbili".

Kwa ufupi: Mtazamo wa Erdoğan wa udugu sio udugu wa Kiislamu! Wito wake wa umoja wa Kiislamu hauko katika umoja ulioonyeshwa na Mtume (saw). Watu, ambao Erdoğan anawahutubia kwa wito wake wa umoja, ni Ruwaibidha, ambao wanajaribu kufifisha neno la Haki la Waislamu, na ambao wanasimama kama vizuizi kwa utukufu (izzah) wa Ummah. Ikiwa Mzayuni muuaji wa halaiki - ambaye anaelewa kumwaga damu za Waislamu nchini Palestina na damu ya watoto wa Gaza na mtu mwingine yeyote isipokuwa yenyewe kama madhumuni yake pekee ya kuwepo - bado anasimama na hata anazidi kuwa mshenzi kwa ujasiri unaokua, basi sababu iko wazi: Ni kwa sababu ya Erdoğan, ambaye, kama vile watawala wa Waarabu, anapigani mamlaka na hadhi ndani ya mifumo ya kirasilimali na sio Uislamu, na ambaye anaegemea upande wa marafiki zake makafiri badala ya kuchukua nafasi katika safu za Ummah.

Ikiwa Erdoğan anataka umoja wa Kiislamu: huko ana mamilioni ya Waislamu, ambao wameungana kwa ajili ya Gaza, wakingojea amri moja kutoka kinywani mwake. Iwapo Erdogan anatamani udugu wa Kiislamu: Huko ana mamilioni ya Waislamu, ambao wanaumia kwa ajili ya kaka na dada zao, na wanaotamani kuwa askari katika jeshi, hilo linatokana na amri yake.

Iwapo Erdoğan angekuwa mkweli, basi angewahutubia Waislamu wenye ikhlasi na sio walinzi wa Sykes-Picot. Kama angekuwa mkweli, basi angependekeza umoja chini ya Qur’an na Sunnah na sio diplomasia ya kibepari kama suluhisho!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu