Ijumaa, 03 Muharram 1447 | 2025/06/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vita vya Amerika na umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran: Kimya cha Watawala na Kujisalimisha kwa Murshed

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza makubaliano kamili kati ya Israel na Iran juu ya usitishaji kamili wa mapigano. Katika jukwaa lake la Kijamii la Truth, Trump alisema: "PONGEZI KWA KILA MTU! Imekubaliwa kikamilifu na kati ya Israel na Iran kwamba kutakuwa na Usitishaji Vita Kamili na Jumla (katika takriban saa 6 kutoka sasa, wakati Israel na Iran zitakapomaliza na kukamilisha misheni zao zinazoendelea, za mwisho!), kwa masaa 12, ambapo Vita vitazingatiwa, VIMEMALIZIKA! Trump alisifu pande zote mbili, akisema: "Misuli, Ujasiri, na Ujasusi kumaliza" mzozo na kusema kwamba ulimwengu na Mashariki ya Kati ndio "WASHINDI halisi". Alimalizia ujumbe wake kwa dua: “Mwenyezi Mungu ibariki Israel, Mwenyezi Mungu ibariki Iran, Mwenyezi Mungu ibariki Mashariki ya Kati, Mwenyezi Mungu ibariki Marekani, na MWENYEZI MUNGU UBARIKI ULIMWENGU!” Tumekomesha vita vikali katika eneo hilo. Wakati huo huo, Reuters ilinukuu chanzo chenye utambuzi kikisema kwamba "Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, alipata idhini ya Tehran ya pendekezo la Amerika la kusitisha mapigano na Israel wakati wa maongezi ya simu na maafisa wa Iran kufuatia mashambulizi ya Iran kwenye Kambi ya Anga ya Al-Udeid nchini Qatar." Shirika la habari la Reuters pia limemnukuu afisa mmoja mkuu wa Iran akisema, "Tehran inakubali kusitisha mapigano na Tel Aviv kupitia upatanishi wa Qatar na pendekezo la Marekani."

Maoni:

Mandhari ya kisiasa yameshuhudia tukio la aibu, lililoadhimishwa na tangazo la upande mmoja la vita dhidi ya Iran na Marekani na umnile la Kiyahudi. Vita hivi vilihusisha mauaji, uharibifu, na ukiukaji wa wazi wa kanuni na sheria zote za kimataifa. Baada ya kukamilisha misheni yao, pande zote mbili—Marekani na umbile la Kiyahudi—zilitangaza kwa upande mmoja kusitisha mapigano, na Iran ikakubali tangazo hili, ikimeza uchungu wa kushindwa bila pingamizi au kusitasita.

Mandhari hii dhahiri ya kisiasa inahitaji maelezo kidogo kuelezea uchungu wake. Marekani imejiteua yenyewe kuwa mfalme wa dunia—hasa ulimwengu wa Kiislamu—na inaona inafaa kuuunda upya kwa njia inayotimiza maslahi yake na kuhakikisha usalama wa umbile la Kiyahudi. Umbile la Kiyahudi lilipewa uhuru wa kuondoa kizuizi chochote, hata kile kidogo zaidi, ambacho kinaweza kuzuia mipango ya Amerika katika eneo hilo.

Ingawa Iran na washirika wake katika kanda hiyo hawakuwahi kuwa kizuizi cha kweli kwa mradi wa Marekani, sura mpya ambayo Amerika inaitaka kwa eneo hili inahitaji kubadilisha sura za zamani, hata kama walikuwa wanyenyekevu na watiifu kwake. Ndio maana viongozi wengi wa kijeshi wa kihafidhina au "wa kivita" nchini Iran waliondolewa, pamoja na wanafizikia wengi wa nyuklia. Kwa kuongezea, vinu vitatu vya nyuklia na maeneo mengi ya kimkakati ya kijeshi na kiuchumi yaliharibiwa, pamoja na miundombinu muhimu ya mafuta.

Uvamizi huu wa Marekani na mkono wake wa kieneo, umbile la Kiyahudi, sio ajabu. Wawili hawa wana kiu isiyoshibishwa ya damu ya Waislamu. Lakini kinachofedhehesha kweli ni jibu kutoka kwa uongozi wa Iran na viongozi wa nchi za Kiislamu katika eneo. Viongozi wa Iran—wa kwanza miongoni mwao, Khamenei—alijisalimisha kwa rais wa Marekani ambaye aliharibu nchi yao, kuwafanya wajane wanawake wao, na kuwafanya watoto wao kuwa yatima. Walikubali kusitishwa kwa mapigano mara moja, kana kwamba ni nchi yao iliyoanzisha vita na kushambulia Amerika na umbile la Kiyahudi sio kinyume chake.

Hii inaashiria kwamba makumi ya viongozi wa kijeshi wa Iran waliouawa na umbile la Kiyahudi hawakuwa na maana hata kidogo kwa Khamenei, kama vile Qassem Soleimani na viongozi wa chama chake nchini Lebanon hawakuwa na maana mbele yake. Kadhalika, zaidi ya mashahidi 70,000 nchini Palestina—ambao kwa niaba yao aliunda kile kinachoitwa “Kikosi cha Quds,” ambacho hakikuwahi kufyatua risasi hata moja dhidi ya wavamizi wa Quds—hawakuwa na thamani yoyote.

Jambo la kufedhehesha pia ni msimamo wa nchi za kieneo na majeshi yao, ambao walifunga anga zao kwa ndege za kiraia huku wakiziacha wazi kwa umbile la Kiyahudi na ndege za kivita za Marekani kulipua na kuua, kisha kuregea salama. Waliona jinai hizi katika nchi jirani kana kwamba hawakuwajali, wakionyesha wazi kwamba watawala wa dola hizi si wasaliti au waoga kuliko watawala wa Iran. Wanangojea zamu yao wenyewe kwenye kichinjio.

Mwenyezi Mungu awalaani watawala hawa wa madhara walioyafunga minyororo majeshi na kuwazuia kuwanusuru ndugu zao wa Iran na Palestina. Wanangojea tu mzunguko wa uharibifu kufikia ardhi nyengine za Kiislamu-kutoka Pakistan hadi Uturuki na kote katika ulimwengu wa Kiislamu.

Umma wa Kiislamu na majeshi yake lazima wachukue hatua kabla haujachelewa. Ni lazima wawaondoe watawala vibaraka wanaoruhusu makafiri wakoloni kutawala rasilimali zetu na kutuvua nguvu zetu za nyuklia, kijeshi na kiuchumi. Juhudi zote za dhati lazima zielekezwe kwenye kuwapindua hawa “wapumbavu wanaoongoza” na kufanya kazi kwa umakini na Hizb ut Tahrir—chama cha kisiasa chenye uwezo wa kutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na kuongoza Umma na majeshi yake katika vita vya ushindi na vya tamkini kama vile Badr, Hattin, na Ain Jalut. Iwapo juhudi za dhati za Ummah na maafisa wake watiifu wa kijeshi hazitaungana ili kuipa ushindi (Nusrah) Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, basi mustakabali chini ya Amerika utakuwa mbaya zaidi kuliko ule ulimwengu wa Kiislamu uliokabiliana nao chini ya Hulagu aliyelaaniwa.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu