Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  1 Jumada II 1446 Na: H 1446 / 059
M.  Jumanne, 03 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maamuzi ya Mkutano wa GCC ni Ushirikiano katika Dhambi na Udanganyifu
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumapili, tarehe 1 Disemba 2024, katika taarifa ya mwisho iliyotolewa na kikao cha 45 cha Baraza Kuu la Baraza la Ushirikiano wa Ghuba iliyoandaliwa na Serikali ya Kuwait, viongozi wa nchi za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (GCC) na wawakilishi wao walitoa wito wa kumalizwa kwa uhalifu wa mauaji na adhabu ya pamoja huko Gaza, uhamishaji wa wakaazi, uharibifu wa vifaa na miundombinu ya raia. Walitoa wito wa kuingilia kati kulinda raia, kusitisha vita, na kufadhili mazungumzo mazito ili kufikia suluhu endelevu, wakisisitiza misimamo yao madhubuti kuhusu kadhia ya Palestina, kukomesha uvamizi huo, na uungaji mkono wao kwa uhuru wa watu wa Palestina juu ya ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu tangu Juni 1967, na kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake, na kuhakikisha haki za wakimbizi, kwa mujibu wa Mpango wa Amani wa Kiarabu na maazimio ya uhalali wa kimataifa. Kuhusiana na Lebanon, viongozi hao walithibitisha mshikamano kamili na Lebanon.

Kwa hivyo, viongozi wa Ghuba walikutana, ingekuwa bora lau kama hawakukutana, kurudia misimamo yao ya dhambi na usaliti. Hawakuguswa na damu ya watu wetu huko Gaza ambayo imemwagika kwa zaidi ya siku 422, wala na mabaki ya mashahidi, wala na vifusi vya uharibifu vilivyojaa Gaza, mitaa yake na vitongoji. Hisia zao hazikuteteleka walipowaona watoto na wanawake wa Gaza wakifa kwa njaa na baridi, na maji yakitoka chini ya hema zao na mbingu juu yao ikiwanyeshea mvua. Matukio haya yote yaliyofanya mawe yaseme na kulia, hayakupata njia ya kuingia nyoyoni mwa viongozi hawa, wala hayakupata nafasi kwao katika maamuzi yao.

Walikusanyika katika madhambi na kufeli, na badala ya kuyakusanya majeshi kukomesha vita vya maangamizi ambavyo jeshi la Kiyahudi linavifanya dhidi ya watu wetu huko Gaza, ili kuwanusuru na kuikomboa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa, ambao wana uwezo wa kufanya. Walitosheka na kutaka kumalizika kwa vita, kukomesha ukaliaji kimabavi na kukomesha jinai za Mayahudi, kana kwamba walikuwa ni upande usioegemea kokote unaozungumza kutoka mbali. Wakati mfumo wa ulimwengu unaoongozwa na Amerika, mkuu wa ukafiri na uhalifu, kwa maoni yao ndio mhusika wa karibu ambao wito na madai yanaelekezwa!

Laiti wangetosheka na madai haya, ili tuweze kusema kwamba walitosheka kwa kuwaangusha watu wetu huko Gaza, sehemu ya Masra ya Mtume (saw) (Safari ya Usiku) na Kibla cha kwanza cha Waislamu. Kusema kwamba walichagua unyonge na hawakuuchanganya na uovu, lakini walifuatisha utelekezaji wao na dhambi na uovu kwa kutilia mkazo wito wa kuanzishwa kwa dola dhaifu ya Palestina ubavuni mwa umbile nyakuzi la Kiyahudi, kwa mujibu wa Mpango wa Amani wa Kiarabu unaoruhusu Mayahudi kunyakua robo tatu ya ardhi iliyobarikiwa na kuhalalisha kikamilifu mahusiano na serikali zilizopo katika nchi za Waislamu, na kwa mujibu wa maazimio ya kimataifa ambayo yalilifanya umbile la Kiyahudi kuwa uhalisia na lenye haki na dhulma. Ama Lebanon, hisa yake ya utelekezaji wao ni kwamba walionyesha tu mshikamano wao nalo!

Watawala wa Ghuba, mithili ya watawala wote wa Waislamu, si chochote ila walinzi wa maslahi ya ukoloni katika nchi zetu. Wanakubaliana tu juu ya kile ukoloni unataka kutoka kwao. Hatua zao ni za dhambi na maamuzi yao ni ya kushutumiwa, na hatutarajii kitu chengine chochote kutoka kwao. Kwa hiyo, majeshi ya Ummah lazima yachukue hatua ya kurudisha mambo mahali pake, ili tuweze kuregea kama Umma mmoja chini ya kivuli cha Imam mmoja anayechunga maslahi na mahitaji yetu, na kuuhamasisha Ummah mzima endapo shubiri moja ya ardhi yake itakabiliwa na uvamizi, hivyo kumaliza zama hizi za giza ambazo Ummah unaishi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ، وَلَا يَتْرُكُ اللهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللهُ هَذَا الدِّينَ، بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ؛ عِزّاً يُعِزُّ اللهُ بِهِ الْإِسْلَامَ، وَذُلّاً يُذِلُّ اللهُ بِهِ الْكُفْرَ»

“Amri kwa yakini itafika kila panapofika usiku na mchana. Haitabaki juu ya uso wa ardhi nyumba ya matofali ya udongo wala hema la manyoya ya ngamia ambayo Mwenyezi Mungu hataingiza dini hii (Uislamu) na kuleta heshima kubwa na fedheha. Heshima ambayo Mwenyezi Mungu ataipa Uislamu na fedheha ambayo Mwenyezi Mungu ataupa ukafiri.”

Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu