Kama Umma Mmoja: Waislamu Wanasimama pamoja na Watu wa Bangladesh Dhidi ya Dhalimu Sheikh Hasina
- Imepeperushwa katika Australia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Watu wa Bangladesh—zaidi ya 92% yao ni Waislamu na sehemu ya mojawapo ya Waislamu wengi zaidi duniani—wamejitokeza katika maandamano ya amani yanayoongozwa na wanafunzi dhidi ya dhalimu Sheikh Hasina. Maandamano ya hivi punde yalizuka baada ya serikali inayoongozwa na Hasina kujaribu kuongeza mgawo wa nafasi za kazi serikalini kwa kuwapendelea wafuasi watiifu wa serikali badala ya wagombea wenye sifa stahiki. Sera hii ni ya hivi punde tu katika mfululizo wa vitendo vya rushwa na uonevu vinavyofanywa na serikali ya Awami League tangu iingie mamlakani mwaka wa 2009.



