Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 410
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa Rais Recep Tayyip Erdogan aliwaambia wanachama wa chama chake kwamba alisikitishwa na kukosa nafasi ya kukutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad katika Mkutano wa hivi karibuni wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai mapema mwezi Septemba. Kauli ya Erdogan ilifuatia ripoti kwamba mkuu wa ujasusi wa Uturuki amekuwa akikutana na mwenzake wa Syria hivi majuzi katikati mwa Septemba.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan kwa uongozi wa Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, akifuatana na Ust. Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Abdul Qadir Abdul Rahman, mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano, Al-Nazir Mukhtar, Shariq Yusef Al-Barbari, Ahmed Bahr, Rahmah Al-Mawla Hajj, na Adam Omar, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walimtembelee Sheikh Al-Reeh Ibn Sheikh Abdullah katika ngome yake huko Taybeh Sheikh Abdul Baqi kisiwani, mnamo Jumatano, 21/9/2022.
Mnamo 2008 vita vilivyokuwa vikiendelea kati ya Ethiopia na Eritrea vilimalizika rasmi. Hata hivyo, kuyumba kwa eneo hilo kunakochochewa na fikra za utaifa kumesababisha serikali ya Ethiopia kuingia katika mienendo ya mizozo na taifa jirani la Tigray.
Zifuatazo ni baadhi ya nukta muhimu kuhusiana na matukio ya hivi sasa nchini Iran kufuatia kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 ambaye inasemekana aliuawa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi la utawala huo, kutokana na kutovaa Hijabu ipasavyo.
Ijapokuwa takriban miezi miwili imepita tangu kuzinduliwa kwa natija nyingi za Chama cha Ushirika wa Kilimo cha Saada, Usajili bado ungali wazi hadi leo kwa kiwango cha elfu kumi kwa kila hisa. Hivyo basi, ni lazima tufafanue uhalisia wa vyama hivyo ambavyo vinakiuka hukmu za Sharia tukufu, na ili kuhakikisha kwamba watu wa Yemen hawaanguki ndani makosa yao hatari.
Mnamo tarehe 24 Septemba 2022 Muttahida Majlis-e-Ulema (MMU), muungano wa makundi ya kidini na kijamii katika Bonde la Kashmir, mnamo Jumamosi walisema majaribio yalikuwa yanaendelea "kuhujumu kitambulisho cha Waislamu wa Kashmir". MMU ilipanga mkutano katika Msikiti wa Jama wa Srinagar ili kujadili hatua za hivi majuzi za kuanza kuimba nyimbo za Kibaniani na Surya Namaskar katika taasisi za elimu za Bonde hilo.
Mnamo siku ya Ijumaa tarehe 16/9/2022, Naibu Waziri Mkuu wa Jordan na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni Ayman Safadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken walitia saini, jijini Washington, mkataba mpya wa maelewano kuhusu uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili kuhusu misaada ya kifedha ambayo Amerika inakusudia kutoa kwa Jordan kwa miaka saba ijayo, ukihakikisha kujitolea kwa Amerika kwa usalama na utulivu wa Ufalme huu.
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Bangladesh leo (23/09/2022) siku ya Ijumaa baada ya Swala ya Ijumaa iliandaa mikutano ya hadhara katika majengo ya misikiti tofauti tofauti ya miji ya Dhaka na Chittagong kupinga kile kinachoitwa sera ya serikali ya kujizuia dhidi ya kuendelea kwa mashambulizi ya makombora na mauaji ya Myanmar kwenye mpaka wa Bangladesh.
Tuliwajia katika barua yetu ya tarehe 19/7/2022 na tukawashauri kwa dhati nyinyi na Waislamu ndani yake. Tumefuatilia matendo, kauli na misimamo yenu muliyotoa, na tumefuatilia matendo na uhalifu wa Mamlaka dhidi ya watu na kadhia ya Palestina.