Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 371
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Swali kuhusu ukusanyaji wa Qur’an tukufu zama za Abubakar As-Swidiq radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee.
Sarafu ya taifa ya Uturuki, lira ya Uturuki, imeporomoka sana katika robo ya mwisho ya mwaka huu, kutoka lira 8.86 za Uturuki kwa dolari moja mwezi Oktoba hadi lira 16.42 za Uturuki kwa dolari moja ya Marekani.
Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, Uturuki ilikuwa ikipitia mgogoro mkubwa wa kiuchumi.
Huku uhusiano ukizidi kuwa mbaya kati ya Beijing na Washington, Rais Joe Biden alitia saini sheria mpya mnamo siku ya Alhamisi (24 Disemba 2021) ya kupiga marufuku bidhaa zinazotengenezwa katika jimbo la Xinjiang la China kwa sababu ya ukandamizaji wa China kwa idadi yake kubwa ya Waislamu wa Uighur walio wachache.
Mwenendo wa kihistoria wa kesi za Hizb ut Tahrir nchini Uturuki umejaa kashfa za kisheria.
BBC iliripoti mnamo tarehe 2 Disemba kwamba miundombinu inayoporomoka ya Afghanistan imesababisha kukaribia kutoweka kwa mfumo wa huduma za afya na ustawi wa jamii.
Waziri wa Mambo ya Nje Shah Mahmood Qureshi mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 16 Disemba 2021, alisema kuwa pamoja na wanachama wa jumuiya ya kimataifa na Taliban kuwepo kwenye jukwaa moja, mkutano wa Disemba 19 wa OIC jijini Islamabad utathibitisha kuwa ni ngazi ya kutafuta suluhisho la janga la kibinadamu nchini Afghanistan.
Pakistan inakabiliwa na uhaba mkubwa wa gesi msimu huu wa baridi unaokuja na serikali tayari inatoa visingizio vyake.
Naveed Butt Alitekwa nyara na maafisa wa Usalama wa Serikali tarehe 11 Mei 2012 Mbele ya Familia yake na majirani zake.