Al Waqiyah TV: Ujumbe kutoka kote Ulimwenguni “Iokoeni Gaza!”
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ujumbe wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kutoka kote Ulimwenguni “Iokoeni Gaza!”
Ujumbe wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kutoka kote Ulimwenguni “Iokoeni Gaza!”
Matembezi ya 66 yalianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 10 Januari 2025 yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuwanusurur watu wa Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka, na kichwa chake kilikuwa “Mapinduzi Yanaendelea Kujikomboa kutokana na Ukoloni na Kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume”
Mnamo tarehe 16 Januari 2025, tovuti ya Al Jazeera ilichapisha masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kuanza leo, Jumapili, Januari 19, 2025. Ilisema: [(Makubaliano ya kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza yalitangazwa katika mji mkuu wa Qatar, Doha kutekelezwa katika hatua 3.
Kenya inashuhudia wimbi kubwa la utekaji nyara na mauaji yanayolenga watu mbalimbali. Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) inaelezea wasiwasi wake juu ya ongezeko la kutisha la utekaji nyara, kupotezwa kwa lazima na mauaji ya kiholela kote nchini. Mwenendo huu ni wa kuchukiza. Baadhi ya makundi ya vijana waandamanaji waliandamana katikati mwa jiji la Nairobi mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 30 Disemba, huku makundi madogo ya watu wengine wakipanga kuketi vikao vya kulaani huku mawingu ya vitoa machozi yakitanda hewani. Waliimba kauli mbiu dhidi ya serikali, huku wengine wakiwa na mabango ya kulaani kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria huku polisi waliokuwa wamepanda farasi wakishika doria karibu na hapo.
Kuongezeka kwa kasi kwa uhasama kati ya Pakistan na Afghanistan katika wiki iliyopita kumesababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa vikosi vya usalama vya Pakistan na makumi ya raia nchini Afghanistan. Raundi hii ya hivi punde ya mapigano ya kuvuka mpaka inatokana na kile Pakistan ilisisitiza kuwa ni jibu lake kwa mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi lenye silaha la Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), ambalo Islamabad ilisema limepata kimbilio katika mpaka wa Afghanistan. Shambulizi la hivi punde zaidi la TTP, mnamo Disemba 21, lilisababisha vifo vya wanajeshi 16 wa Pakistan.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwatangazia wafuasi na wageni wake katika tovuti za Afisi Kuu ya Habari kuanza tena uchapishaji wa Al-Raya, ambalo lilikuwa linachapishwa na Hizb ut Tahrir mnamo 1954.
Katika mwezi wa Rajab Mtukufu mwaka huu 1446 H - 2025 M, tunakumbuka kumbukumbu mbaya ya miaka 104 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Waarabu na Waturuki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake, na Maswahaba zake watukufu na waliobarikiwa, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Kutokana na hili, Hizb ut Tahrir inaandaa amali mbalimbali za umma katika nchi zote ambazo inaendesha shughuli zake za kuwahamasisha Waislamu kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.