Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 533
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Utawala wa Jordan na kundi la watu wake wakati wote wa vita vya Kiyahudi dhidi ya Gaza walikuwa na bado wangali wanatetea kutowanusuru watu wa Gaza kijeshi, na angalau sio kufutilia mbali makubaliano ya udhalilishaji na aibu na umbile la Kiyahudi, lakini kwa busara na hekima na ujanja wa kisiasa hii ni hatua na udhoofishaji wa amani, usalama na chemchemi ya utulivu ambayo Jordan inaishi ndani yake. Mfalme alifikiri kwamba Uingereza ilimuamuru kurukuu na kujibu ajenda ya Amerika ambayo imelitawala eneo hilo tangu aingie madarakani, kufuatia mbinu ya baba yake, na kile ilichomuagiza kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya ulinzi nayo mwaka 2021 ambayo yanahujumu kila maana ya ubwana wa nchi yoyote, na kuifungua nchi kwa ujumla kwa kambi za Amerika pekee na viwanda na vikosi vyake.
Mnamo tarehe 30 Disemba, iliripotiwa kuwa mtoto wa 6 waliganda hadi kufa mjini Gaza ndani ya wiki mbili kutokana na hali ya baridi inayovumiliwa na wakimbizi wa Kipalestina katika mahema ya muda, waliohamishwa kutoka kwa nyumba zao kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukanda huo na uvamizi wa Kiyahudi. Ali al-Batran mwenye umri wa mwezi mmoja alifariki siku moja baada ya kaka yake pacha, Jumaa al-Batran, huko Deir el-Balah. Baba yao, Yahya Muhammad al-Batran, alisema kuwa Jumaa alipatikana kichwa chake kikiwa kama “donge la barafu”. Nariman, mama wa Sila Mahmoud al-Fassih mwenye umri wa siku 20, ambaye pia alifariki kutokana na kupungua kwa joto la mwili, alielezea kumkuta mtoto wake akiwa rangi ya bluu na kuuma ulimi wake huku damu ikimtoka mdomoni. Zaidi ya watu milioni 1.6 wa Gaza wamelazimishwa kuingia kwenye makaazi ya muda, wakiishi katika mahema hafifu ambayo hayatoi ulinzi kutokana na hali ya hewa ya baridi kali.
Tunapokaribia kumbukumbu ya mwaka wa 104 wa kuvunjwa kwa Khilafah, Umma wa Kiislamu unaendelea kupokea habari za ukandamizaji kutoka kwa maadui wake kila mahali, kuanzia Palestina hadi Syria, Sudan, Misri na China, ambako Waislamu wa Uyghur wanavumilia mateso na vikwazo vikali katika kila nyanja ya maisha yao.
Ulimwengu umefuatilia machafuko ya Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambayo yalilenga watu waliokimbia makaazi yao na wakaazi kutoka Sudan Kaskazini. Matukio haya yalichochewa na ripoti zinazowatuhumu wanajeshi wa Sudan kwa kuwaua watu kutoka Sudan Kusini huko Wad Madani baada ya jeshi kuutwaa tena mji huo. Kulingana na gazeti la ‘Sudan Tribune’, Wasudan watatu waliuawa mjini Juba, na wengine saba kujeruhiwa.
Chini ya mada hii, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilifanya kikao chake cha kawaida, Kikao cha Masuala ya Umma, ambacho mwezi huu, mwezi wa Rajab, kilifanyika kukumbuka kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah, inayofikisha miaka 104 tangu kuanguka kwake katika mwezi wa Rajab 1342 H.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa leo, tarehe 27 Rajab 1446 H, sawia na tarehe 27 Januari 2025 M, katika Soko Kuu la Port Sudan chini ya kichwa: “Kubadilisha Hukmu za Mwenyezi Mungu ni Hatari Kubwa na Madhara Makubwa.”
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunafuraha kuwaalika wanataaluma wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wanaopenda masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika Kikao cha Masuala ya Ummah cha kila mwezi, ambao mwezi huu kimepewa kichwa: Sera ya Trump kwa Mashariki ya Kati… na Hasa Sudan
Tawala za ulimwengu wa Kiislamu zinatoa wito wa kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka huu, licha ya kuwa wametambua uwepo wa umbile linaloinajisi ardhi iliyobarikiwa ya Isra na Mi’raj. Wamesimama kando, wakishuhudia mito ya damu ya Wapalestina ikitiririka, mabomu yaliyosababisha nyumba kuwa vifusi, na uharibifu ulioharibu vitongoji, mazao, na vizazi. Wametazama huku hofu ikiwashika wazee na vijana, huku njaa isiyo kifani ikiwasibu, na huku baridi ikigandisha miguu na nyoyo za watu.
Hatimaye, baada ya Mauaji ya Kutisha na Uharibifu wa Kutisha uliofanywa na Mayahudi mjini Gaza