Mateso ya Wanawake Kwa Sababu ya Vita Yanathibitisha Haja ya Haraka ya Mfumo wa Kiwahyi ili Kuyapangua Machafuko haya
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika taarifa moja ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mnamo tarehe 6/12/2023, kuhusu vita vya Sudan, ambapo alishutumu jeshi pamoja na Vikosi vya Msaada wa Haraka, alisema: "RSF na wanamgambo washirika wao wamewahangaisha wanawake na wasichana katika maeneo mbalimbali ya Sudan, kupitia unyanyasaji wa kingono, kuwashambulia majumbani mwao, kuwateka nyara kutoka mitaani, na kuwalenga wale waliojaribu kukimbilia usalama nje ya mpaka...”