Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan Wakutana na Ustadh Al-Taher Hassan Al-Mohami
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan Wakutana na Ustadh Al-Taher Hassan Al-Mohami.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan Wakutana na Ustadh Al-Taher Hassan Al-Mohami.
Mkutano huo ulijadili hali ya kisiasa nchini, vita vinavyoendelea, na hali ya mvutano kati ya vipote vya watu wa Sudan, kutoka kwa mapigano ya kikabila, migogoro kwa msingi wake, na maafa ambayo imeleta juu ya nchi na watu, na kwamba njia ya kutoka humo inawezekana tu kwa msingi wa hukmu za Uislamu mtukufu na sheria yake.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Sheikh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na akiwemo Abdullah Hussein, Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, na Mohammed Mukhtar, Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, ulikutana na Sheikh Othman Arefa, mjumbe wa Kamati ya Wanazuoni wa Jimbo la Bahari Nyekundu na Imam wa Msikiti wa Ibn Masoud, mnamo siku ya Jumamosi, 25 Shawwal 1445 H sawia na 4 Mei 2024 M, katika Afisi ya Hizb ut Tahrir Wilayah ya Sudan. katika mji wa Port Sudan.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, ulioongozwa na Ustadh Yaqoub Ibrahim, na mwanachama: Ustadh Mwanasheria Ahmad Abkar, Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, na Ustadh Suleiman Al-Dasis, na Ustadh Daoud Abdullah, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walimtembelea, Bw. Azraq Tilfone, Nazir (Kiongozi Mkuu) wa Makabila ya Nuba nchini Sudan, katika makaazi yake mjini Port Sudan mnamo siku ya Ijumaa, 24 Shawwal 1445 H sawia na 3/5/2024 M.
Mgogoro wa Sudan, vita vinavyoendelea na matokeo yake yalijadiliwa. Pande zote mbili zilisisitiza umuhimu wa suluhisho kuwa mbali na uingiliaji kati na ajenda za kutoka nje, na kwamba suluhisho lazima litokane na itikadi tukufu ya Uislamu.
Kwa msaada na muongozo wa Mwenyezi Mungu, leo, Jumapili, tarehe 7 Ramadhan 1445 H, sawia na tarehe 17 Machi, 2024, Afisi ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan imezinduliwa mjini Port Sudan (mtaa wa Al-Athmah), kusini-mashariki mwa uwanja. Itatumika kama nguzo ya kueneza fikra za Kiislamu, jukwaa la thaqafa ya Kiislamu, kitovu cha utambuzi wa kisiasa, na nukta kianzilishi cha ubebaji ulinganizi kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya utume.
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya matembezi makubwa katika mji wa Gadharef, baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 28 Rajab 1445 H, sawia na tarehe tisa Februari 2024 M
Baada ya kuridhika na Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan inamuomboleza kwa masikitiko makubwa zaidi aliyesamehewa, Mwenyezi Mungu akipenda:
Sheikh Abdul-Fattah Othman Muhiyidin
Waziri wa Fedha Jibril Ibrahim, kwa mara ya tano mfululizo, aliongeza kwa ujasiri bei ya dolari ya forodha, ambayo ilianza kuongezeka mnamo Juni 2021, kutoka pauni 28 hadi pauni 370, kisha hadi pauni 445, kisha hadi pauni 564, kisha hadi pauni 650.
Mwanamke mmoja mdogo kutoka Sudan alishiriki katika mashindano yanayojulikana kama ‘Miss World’, ushiriki uliosherehekewa na Yaser Arman, kiongozi katika Baraza Kuu la Uhuru na Mabadiliko akitoa maoni yake kwa ujanja, licha ya athari kubwa ya utamaduni wa uokoaji dhidi ya ubunifu, urembo, na wanawake, Tibah Diab, mshiriki kijana, alionyesha ujasiri na ufahamu, akisubutu kushiriki katika mashindano ya urembo na kujaribu kuakisi sehemu ya turathi, utamaduni, na utambulisho wetu.