Ijumaa, 27 Rajab 1447 | 2026/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Watoto wa Afghanistan na Unafiki wa Kimagharibi

Tangu utawala wa Marekani uondoke Afghanistan na serikali ya Taliban kuchukua madaraka, maamuzi ya nchi za Magharibi yalianza kuongezeka, hasa baada ya kundi la Taliban kuchukua maamuzi ambayo Magharibi inayaona kuwa hayaendani na hadhara na mtindo wake wa maisha, kama vile kulazimisha niqab kwa wanawake na kutenganisha madarasa kati ya wanaume na wanawake, pamoja na maamuzi mengine.

Soma zaidi...

Kipindupindu Kinawaua Watu wa Syria, Hivyo Iko Wapi Dola ya Kuwanusuru?!

Wizara ya Afya ya Utawala wa Syria ilitangaza mnamo Jumatatu kuwa mkurupuko wa kipindupindu katika maeneo kadhaa umewauwa watu 29, vifo na majeruhi vilikolea katika jimbo la kaskazini la Aleppo, ambapo watu 25 walithibitishwa kufariki, na maelfu kadhaa ya visa vinavyoshukiwa kuripotiwa kote nchini kuanzia Septemba 19, kulingana na data iliyopatikana na chama cha misaada kutoka Kitengo cha Afya cha Serikali ya Syria (GoS), Idara ya Kibinafsi ya Mamlaka ya Afya ya Mitaa, Kaskazini na Mashariki mwa Syria.

Soma zaidi...

Lau Tungekuwa na Ngao ya Ulinzi na Imam, Mayahudi Wasingesubutu Kunyakua Ardhi Yetu na Kuifisidi

Mnamo tarehe 9/23/2022, Al Jazeera Kiingereza ilichapisha ripoti kuhusu mateso ya watu wa Masafer Yatta [Palestina] kutokana na mashambulizi ya walowezi. Ripoti hiyo ilinukuu ushahidi wa wanawake wa eneo hilo, waliozungumzia mateso yao na familia zao kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wavamizi na makundi ya walowezi, ambapo wanapigwa, kupigwa risasi za moto, kushambuliwa kwa gesi na kukamatwa.

Soma zaidi...

Watoto Wapendwa wa Ash-Sham Wafariki Baada ya Boti za Wakimbizi Kuzama. Je, Tunapoteza Wangapi Zaidi Bila Khilafah?!

BBC iliripoti mnamo tarehe 23 Septemba 2022 kwamba wakimbizi wahamiaji 71 walipatikana katika mashua inayozama nje ya pwani ya Syria. Makumi wameripotiwa kufariki. Watu 20 kati ya walionusurika walipelekwa katika jiji la Tartus kutibiwa hospitalini. Wanawake na watoto wa Lebanon, Syria na Wapalestina walikuwa miongoni mwa watu 120 hadi 150 waliokuwemo ndani.

Soma zaidi...

Kambi ya Rukban, Khiyana na Kurudi kwa Waliohamishwa katika Enzi ya Iliyopita

Shirika la Kuchunguza Haki za Binadamu la Syria liliripoti kwamba familia 4 ziliondoka kwenye kambi ya al-Rukban, iliyoko kwenye mpaka wa mashariki wa Syria na Jordan na Iraq, na limenakili kuondoka kwa familia 18 na vijana 19 katika makundi sita hadi maeneo yanayodhibitiwa na serikali,

Soma zaidi...

Bangladesh Yazifunga Shule za Waislamu wa Rohingya Yatishia Kuwavua Kitambulisho Chao na Kuwahamisha hadi Kisiwa cha Mbali Endapo Zitafunguliwa

Maafisa nchini Bangladesh wanatishia kuwanyang'anya wakimbizi wa Rohingya hati zao za utambulisho na kuwahamisha kwa nguvu hadi katika kisiwa cha mbali ambacho hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara, endapo watakiuka marufuku jumla kwa shule walizozianzisha, kulingana na shirika la Human Rights Watch.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu