Jumatano, 07 Shawwal 1447 | 2026/03/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Pongezi kwa Mnasaba wa Idd al-Adha al-Mubarak Kutoka Ardhi ya Zaitouna, Tunisia, hadi Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Huku sauti za mahujaji kwenye nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu zikipaa kwa mwito wa Mwenyezi Mungu, sauti za watu wa Gaza zimepaa tangu Kimbunga cha Aqsa katika kumwita Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, vikosi vyote vya ukafiri na dola za kihalifu kutoka Magharibi, ambazo zina chuki dhidi ya Uislamu na watu wake, zinakula njama dhidi yao ili kuliokoa umbile katili la Mayahudi na kuupiga vita mradi mtukufu wa Kiislamu unaotokana na itikadi yetu, na kumaliza matamanio yetu ya utu na wokovu kupitia kutabikisha sheria ya Mola wetu.

Soma zaidi...

Maadui wa Mapinduzi Wanaogopa Vuguvugu la Ummah na Wanaonya kuhusu Kupoteza Udhibiti

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, ameonya juu ya kuongezeka kwa taharuki nchini Syria, na kulitaja kuwa eneo jengine hatari linaloonyesha mwelekeo wa kupamba moto. Amefahamisha kuwa kadhia ya Syria inahitaji mkabala wa kina ili kufikia suluhu endelevu. Kauli hii aliitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (GCC), uliofanyika jijini Doha mnamo tarehe 9 Juni 2024.

Soma zaidi...

Pongezi kwa Mnasaba wa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd

Maumivu yetu yanazidi tunaposhuhudia jinai hii kwa macho yetu wenyewe, huku majeshi ya Umma wa Kiislamu yakibaki bila kuchukua hatua yoyote, yakiwa hayana mwelekeo wa kuwasaidia ndugu zao wanaodhulumiwa. Vilio vya wafiwa na machozi ya watoto haviwasumbui, na majeshi haya bado hayajibu kwa sauti ya juu kabisa “Labbaik Allahumma Labbaik” katika kuitikia mwito wa Mola wao wa jihad na kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa. Je, udhaifu na udhalilifu umefikia kiwango hiki?

Soma zaidi...

Kesi ya Kisiasa Inafichua Uungaji Mkono wa Denmark kwa Uvamizi wa Mauaji ya Halaiki

Serikali ya Denmark inaendelea na uungaji mkono wake wa dhati kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza, ambayo yameitia hofu kila nafsi adhimu katika sayari hii, na kuwaamsha watu kuona kwamba vima vinavyodaiwa vya dola za Magharibi vimezikwa na maiti hizo za maelfu ya wanawake na watoto chini ya magofu ya Gaza. Haki za binadamu, haki ya kuishi na kujiamulia, haki za wanawake na ustawi wa mtoto - yote haya yanatupwa chini ya tingatinga la Uzayuni na wanasiasa na mamlaka, ambao kwa hivyo wanaonyesha unafiki wao wa hali ya juu na kufichua jinsi gani "vima" hivi kivitendo ni ala tu za kisiasa.

Soma zaidi...

Mbweha ni Mbwa Mwitu Anayetuma Maua… Mbweha Ana Hila Nyingi…

Aliyekuwa balozi wa Marekani katika umbile la Kiyahudi, Martin Indyk, mnamo Alhamisi tarehe 20 Juni aliamua kuondoa mwaliko kwa Waziri Mkuu wa Kiyahudi Benjamin Netanyahu kutoa hotuba mbele ya Bunge la Congress. Hii ni ili aombe radhi kwa kuutuhumu utawala wa Rais Joe Biden kwa kuinyima silaha “Israel,” huku vyombo vya habari vya Kiyahudi vikisema kuwa Netanyahu anapendelea makabiliano ya hadharani na Washington.

Soma zaidi...

Tanzania na Janga la Utegemezi

Jumapili ya tarehe 02 Juni, Juni 2024, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Korea Kusini zilitia saini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jijini Seoul. Mikataba hiyo ilijumuisha mkopo wa dolari bilioni 2.5 (Tsh trilioni 6.5) uliotolewa na Korea Kusini chini ya Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini (EDCF) kwa ajili ya miradi mbalimbali ya miundombinu.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu