Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 416
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya makubaliano ya mnamo tarehe 15 Oktoba 2022 kati ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Tunisia katika ngazi ya wataalamu wa ufadhili wa dolari bilioni 1.9 kwa kipindi cha miaka 4, sisi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, tunawahutubia, tukiwashauri na kuwaonya juu ya matokeo ya mkataba huu na madhara yake kwa nchi na wananchi, hasa kwa vile mumedai, kwa zaidi ya mara moja, kwamba mumekuja kurekebisha yale yaliyofisidiwa na serikali zilizopita!
a) Je, kuna kitu katika Uislamu kama "thamani ya soko la kampuni" mbali na suala la hisa katika urasilimali?
b) Je, alama ya biashara ina thamani ya kutathminiwa wakati kiwanda kinauzwa?
c) Je, alama ya biashara ni ya kiwanda au kampuni, yaani, ikiwa kampuni itabaki na kuuza kiwanda chake kimoja au laini ya uzalishaji kwa moja ya vifaa vyake, ni nini kinachozingatiwa katika kukadiria bei?
d) Katika tukio la kampuni kuvunja, nini kitatokea kwa alama ya biashara?
Maafisa wa Marekani wameripotiwa kuionya serikali ya Ukraine kwa faragha kwamba inahitaji kuashiria uwazi wa kufanya mazungumzo na Urusi. Maafisa jijini Washington wameonya kwamba "uchovu wa Ukraine" miongoni mwa washirika unaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa Kyiv itaendelea kufungwa kutokana na mazungumzo, Washington Post liliripoti.
Shirika la habari la NPR liliripoti kwamba mfungwa mzee zaidi katika Guantanamo Bay aliachiliwa huru akiwa na umri wa miaka 75 na hivyo kupunguza idadi ya watu hadi 35. Saifullah Paracha alirudishwa nyumbani katika nchi yake ya asili ya Pakistan katika wiki ya mwisho ya Oktoba 2022. Kuachiliwa huru huku kuliidhinishwa kwa msingi wa ukweli kwamba hakukuwa na ushahidi wowote wa kuzuiliwa kwake na kwamba hakuwezi kuwa na uhalali zaidi wa kumweka gerezani.
Takriban watu 100 wameuwawa na wengine 300 kujeruhiwa kwenye shambulizi la mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud alisema.
Mapema Oktoba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtakatifu Burhanuddin alitembelea mkoa wa Visiwa vya Riau, ambao ni eneo la mpakani nchini Indonesia. Aliomba kwamba upande wa mashtaka kwa kesi za Ulanguzi wa Dawa za Kulevya na Binadamu katika Visiwa vya Riau utoe athari ya kuzuia wahalifu katika eneo la Visiwa vya Riau (Kepri). Alitaka vifungu viweze kuongezwa.
Rais wa China Xi Jinping na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz mnamo Ijumaa walilaani vitisho vya kutumia silaha za nyuklia nchini Ukraine, huku Scholz akionya kwamba Urusi inakabiliwa na hatari ya "kuvuka mstari" katika jumuiya ya kimataifa kwa kutumia nguvu za kinyuklia.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ajenda katika Jumba la Rais, Rais Erdoğan alisema, “Mataifa imara yanajumuisha familia imara. Kama sharti la hadhara yetu ya zamani, sisi ni taifa linaloundwa kutokana na familia imara. Sio mahali pa mtu yeyote kuharibu muundo wa familia ya taifa hili. Tutalinda muundo wa familia yetu dhidi ya kila aina ya upotovu.”
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa umeelezea hatua pana za mageuzi, ikiwemo kuleta nidhamu katika sekta ya fedha na kuongeza ukusanyaji wa mapato, kwa Bangladesh kupata mkopo wa dolari bilioni 4.5. Hatua hizo zilijadiliwa wakati wa msururu wa mikutano kati ya ujumbe uliozuru wa IMF na mashirika mbalimbali ya serikali na idara za Bangladesh.