Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 417
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Msukosuko wa sasa wa kisiasa nchini Pakistan kimsingi haukufungika kwenye mzozo kati ya PTI ya Imran Khan na serikali ya PDM. Haijafungika hata kwenye mvutano kati ya vikundi vya jeshi lenye nguvu. Msukosuko wa kisiasa una athari pana zaidi. Inapanuka ili kuwezesha malengo na maslahi ya Marekani katika eneo hili, kwa wakati huu. Hii ni bila kujali kama uwezeshaji huu ni wa kubuniwa kimakusudi, au kwa matokeo ya bahati mbaya, ya kusikitisha.
Katika siku chache, timu ya taifa ya kandanda ya Denmark itasafiri hadi Qatar kuiwakilisha Denmark katika Kombe la Dunia 2022. Wachezaji wa Denmark watacheza wakiwa na nguo nyeusi, ambazo zitaashiria bendi ya maombolezi ambayo inaashiria kutoridhika na serikali nchini Qatar na ambayo inaashiria kwamba Denmark anahudhuria mazishi.
Teen Vogue alitoa hadithi yenye kichwa “Kuvaa Hijab Kunapaswa Kuwa Chaguo la Kibinafsi, Wanawake wa Kiislamu wa Kimarekani Wanasema.” Madhumuni ya makala hayo ilikuwa ni kukuuza utofauti na ujumuishwaji na kutoa sauti kwa yale yanayoitwa makundi yaliyotengwa.
WAZIRABAD: Waziri Mkuu wa zamani na mwenyekiti wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) Imran Khan na viongozi wengine kadhaa wa PTI walijeruhiwa baada ya mtu mmoja kufyatua risasi karibu na kambi ya mapokezi ya PTI huko Allahwala Chowk wakati wa maandamano marefu ya chama hicho, ARY News iliripoti mnamo Alhamisi.
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Syria iliandaa maandamano katika mji wa Atarib viungani mwa Aleppo
Mnamo tarehe 11/09/2022, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kiliwasilisha mjadala kuhusu "Shambulizi dhidi ya Hijabu barani Ulaya", ambapo washiriki walizungumza kuhusu vikwazo ambavyo wanawake wa Kiislamu katika nchi za Magharibi wanakumbana navyo, ambao ulimkasirisha mwandishi wa habari Jean Chichizola kiasi kwamba aliandika makala yaliyochapishwa mnamo tarehe 19/10/2022 kwenye Gazeti la Le Figaro, yenye kichwa "Ufaransa inatuhumiwa kutaka "kuuondoa Uislamu" kwa vijana wa Kiislamu.
Mnamo Alhamisi asubuhi, Oktoba 27, 2022, Benki Kuu ya Misri ilipandisha viwango vya riba kwa pointi 200, wakati wa mkutano wa kipekee, hivyo kiwango cha maregesho ya amana na mikopo ya usiku mmoja kikawa asilimia 13.25 na asilimia 14.25, mtawalia, na taarifa ya Benki Kuu.
Mji wa Jasim ulizingirwa mwezi Agosti mwaka wa 2022. Kisingizio cha hilo kilikuwa uwepo wa chembechembe za ISIS katika mji huo. Mji huo baadaye ulivamiwa mnamo Oktoba; wengi waliuawa wakati wa uvamizi huo. Kabla ya hapo, mji wa Tafas ulishuhudia mandhari hiyo hiyo, na utawala wa kihalifu ulijaribu kuuvamia na kuzua mifarakano miongoni mwa wakaazi wake.
Rais wa Tunisia, Kais Saied, akimpokea katika Kasri la Carthage, mnamo Ijumaa, Novemba 4, 2022, Dkt. Abdel Rahman bin Abdullah Al Hamidi, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfumo wa Fedha wa Waarabu, mbele ya Mkurugenzi wa Benki Kuu, Marwan Al Abbasi.