Enyi Waislamu: Msiruhusu Ardhi Zenu Kuwa Jukwaa la Majeshi ya Wakoloni!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Serikali ya Uingereza imetangaza kupelekwa kwa silaha ya gharama nafuu ya kupambana na droni katika operesheni zake za kijeshi Mashariki ya Kati. Katika taarifa yake, ilisema, “Mfumo mpya sasa umepelekwa katika kumbi za operesheni katika eneo la Mashariki ya Kati.” Pia ilisema kwamba Uingereza “itachangia kwa droni, ndege za kivita, na manuari katika misheni ya kimataifa ili kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz.”



