Maamuzi ya Mkutano wa GCC ni Ushirikiano katika Dhambi na Udanganyifu
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Jumapili, tarehe 1 Disemba 2024, katika taarifa ya mwisho iliyotolewa na kikao cha 45 cha Baraza Kuu la Baraza la Ushirikiano wa Ghuba iliyoandaliwa na Serikali ya Kuwait, viongozi wa nchi za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (GCC) na wawakilishi wao walitoa wito wa kumalizwa kwa uhalifu wa mauaji na adhabu ya pamoja huko Gaza, uhamishaji wa wakaazi, uharibifu wa vifaa na miundombinu ya raia. Walitoa wito wa kuingilia kati kulinda raia, kusitisha vita, na kufadhili mazungumzo mazito ili kufikia suluhu endelevu, wakisisitiza misimamo yao madhubuti kuhusu kadhia ya Palestina, kukomesha uvamizi huo, na uungaji mkono wao kwa uhuru wa watu wa Palestina juu ya ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu tangu Juni 1967, na kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake, na kuhakikisha haki za wakimbizi, kwa mujibu wa Mpango wa Amani wa Kiarabu na maazimio ya uhalali wa kimataifa. Kuhusiana na Lebanon, viongozi hao walithibitisha mshikamano kamili na Lebanon.