Kampeni ya Kimataifa na Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina Kuyaita Majeshi ya Waislamu Kuwaokoa Wanawake na Watoto wa Gaza na Kuikomboa Ardhi Yote ya Al Aqsa
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Huku ulipuaji mabomu wa kikatili wa Gaza ukiendelea na umbile uaji la 'Kizayuni', ni wanawake na watoto ndio wanaohimili makali ya mauaji haya ya halaiki, wakijumuisha 70% ya wale waliouawa. Mvua ya mabomu kwenye majengo ya makaazi, maeneo ya hifadhi, shule, hospitali na vitongoji yamesababisha Gaza kuwa makaburi kwa wanawake na watoto, huku watoto zaidi ya 4500 na wanawake 3000 wakiuawa tangu Oktoba 7.