Kwa kukosekana Khilafah, Watoto wa Ummah wetu nchini Iraq Wanaanikwa kwa Hofu za Utaifa
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 29 Septemba 2022, shirika la Habari la ‘Arab News’ liliripoti juu ya mashambulizi ya droni yaliyoanzishwa na Iran kwa kile kinachoitwa mawakala wa waasi wa Kikurdi katika eneo hilo. Milipuko ilitokea katika mji wa Irbil, Kurdistan ya Iraq na kushambulia shule moja iliyokuwa imejaa wanafunzi. Waandishi wa habari katika eneo la tukio walisambaza picha za watoto wa shule waliotapakaa damu katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq.